Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Beatrice Mwaipaja – Dhahabu

Audio

Video | Audio: Beatrice Mwaipaja – Dhahabu

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu leo kupitia tovuti yako pendwa ya kikristo nimekusogezea video iitwayo Dhahabu kutoka kwa mwanadada Beatrice Mwaipaja, video ikiwa imeongozwa na director Jackson Joaqim kutoka studio za Blessing Studio na muziki ukiwa umetayaarishwa na mikono ya prodyuza Maka-Rhythm.

Dhahabu ni wimbo uliobeba ujumbe wa kukupa hamasa na nguvu ya kuendelea mbele hata kwa kipindi ambacho unahisi kuchoka na kukata tamaa ndani ya nafsi yako, kupitia wimbo huu mwimbaji Beatrice Mwaipaja anatukumbusha kuwa kila pito tunalopitia ni ishara ya ushindi kwa siku zijazo hivyo hutupaswi kukata tamaa kwakuwa Mungu alituumba kwa mfano wake hivyo sisi ni mfano wa thamani ya dhahabu ambayo haiwezi kung’aa mpaka ipitishwe kwenye moto mkali, vivyo hivyo katika maisha yetu ya kawaida tunakuwa tunapitia mapito magumu sana ambayo yanaweza kusababisha kutokuona ukuu na upendo wa Mungu kwetu lakini tunapaswa kutambua kuwa ushindi wetu ni lazima kwa yeyote amtegemeaye Mungu, kwakuwa wewe ni Dhahabu.

Kwa mujibu wa Beatrice Mwaipaja alisema haya kuhusu ujumbe ulio katika wimbo huu:

Huu ni wimbo wangu mpya ambao unaitwa DHAHABU, ni wimbo wenye kutia Moyo kwa ambao wamedharaulika na kuteswa na maneno ya Binadamu. Kama Dhahabu uwa inapita kwenye Moto ili kuwa Dhahabu hivyo nasi lazima tupite kwenye magumu ili tuifikie Ile NEEMA ambayo Mungu ametuandalia.” – Alisema Beatrice Mwaipaja.

Nina hakika utabarikiwa na kuinuliwa, Karibu kutazama, na kupakua wimbo huu ambao nina imani utabarikiwa.

[easy_media_download url=”https://gospomedia.com/wp-content/uploads/2018/03/Beatrice-Mwaipaja-Dhahabu-1.mp3″ text=”Download Audio” force_dl=”1″]

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko mbalimbali na kama unahitaji kufanya kazi na mwimbaji Beatrice Mwaipaja wasiliana naye kupitia:
Namba za simu/WhatsApp: +255 654 345 737
Facebook: Beatrice Mwaipaja
Instagram: @beatrice_mwaipaja
YouTube: Beatrice Mwaipaja

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

More in Audio

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,131 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top