Video | Audio: Angel Benard - Utukumbuke - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Angel Benard – Utukumbuke

Audio

Video | Audio: Angel Benard – Utukumbuke

Moja ya kati ya video zilizokuwa zinasubiliwa kwa shauku kubwa na wafuatiliaji wa muziki wa Injili wakiwemo wadau na mashabiki wa muziki huu ni hii video iitwayo Utukumbuke kutoka kwa mwanadada anayependwa zaidi katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla wake huyu si mwingine bali ni Angel Benard ambaye siku ya leo ameachia rasmi video ya wimbo wake mpya Utukumbuke.

Video ya wimbo huu imeongozwa na Kwetu Studios na muziki ukiwa umetayaarishwa na studio za Still Alive zilizopo nchini kenya.

Utukumbuke ni wimbo unaoelezea maombi kwa Mungu juu ya yale tunayoyahitaji katika maisha yetu, Wanadamu leo tumekuwa tunapita katika majaribu magumu na shida mbalimbali ambazo kwa wakati mwingine zinatufanya tuwe mbali na uso wa Mungu lakini mwimbaji Angel Benard kupitia wimbo huu anatukumbusha kuwa licha ya kila majaribu na shida zote tunazopitia bado Mungu ana nafasi ya kutusikiliza kwa kile tunachohitaji kutoka kwake kwa maana mkono wake sio mfupi usiokoe na sikio lake sio zito asisikie yeye ni mwanzo na mwisho kwake hakuna linalomshinda Bwana Yesu.

”ISAYA 62:6-7 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha BWANA msiwe na kimya; Wala msimwache akae kimya, mpaka atakapo ufanya imara Yerusalemu, nakuufanya kuwa sifa duniani.” – Angel Benard

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi, mialiko ya huduma wasiliana na muimbaji Angel Bernad kupitia
Simu/WhatsApp: +255 652 887 050 au +255 759 444 488
Facebook: Angel Benard
Twitter: @angelbenard
Instagram: @angelbenardofficial
YouTube: Angel Benard

Like us on facebook >> GOSPO MEDIA  Follow us on instagram >> @gospomedia

Advertisements

More in Audio

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top