Video | Audio: Paul Clement Feat. Frida Felix - Jina la Yesu - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Video | Audio: Paul Clement Feat. Frida Felix – Jina la Yesu

Video

Video | Audio: Paul Clement Feat. Frida Felix – Jina la Yesu

Kwa mara nyingine tena katika mwaka 2018 Paul Clement moja kati ya waimbaji wanaofanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao Jina la Yesu akiwa amemshirikisha mwanadada mwenye sauti ya pekee anayefahamika kwa jina la Frida Felix, video ikiwa imeongozwa na studio za Fisher Records ikishirikiana na Kwetu Studios, na muziki ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Fishers Records chini ya mikono ya prodyuza Taz akishirikiana na John Marco.

Jina la Yesu ni wimbo wa sifa unaomtukuza Mungu kwa namna ya kipekee kwa kudhihirisha nguvu na uweza wa mwanaye wa pekee aliyemtoa kwa ajili ya kutetea maisha yetu na kutuweka mbali na uovu, jina lake Yesu bado linaishi mpaka sasa na limekuwa likitenda mambo makubwa na ya ajabu katika maisha yetu kwa namna ambayo hatuwezi kueleza, hakuna jina lipitalo jina la Yesu Kristo.

”Jina la YESU KRISTO, ni jina juu ya majina yote, kila goti lipagigwa, na kila ulimi utakiri kwamba Kristo ni Bwana.” – Paul Clement

Nina imani kuwa utafurahia na kubarikiwa kwa kutazama na kusikiliza wimbo huu ambao kwa hakika utatenda muujiza kwako mwana wa Mungu kupitia jina la Yesu, Ameen!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya kihuduma wasiliana na mwimbaji Paul Clement kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 625 661 862 au +255 719 367 002
Facebook: Paul Clement
Instagram: @paulclement_official
YouTube: Fisher Records
Email: fisherrecordstz@gmail.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements

More in Video

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top