Connect with us

Gospo Media

Video: Fabrice J. Prince – Amani ya Moyo

Video

Video: Fabrice J. Prince – Amani ya Moyo

Kutoka jijini Virginia, nchini marekani mpaka Tanzania leo nimekusogezea video nzuri, utakayoifurahia na kukubariki kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili mwenye asili ya Tanzania anayeishi nchini marekani anayefahamika kwa jina la Fabrice J. Prince.

Video ya wimbo huu imeongozwa na director mahiri kutoka mjini chicago, marekani anayefahamika kwa jina la Innocent kutoka studio za Ganza Image na wimbo ukwa umetayaarishwa na prodyuza mahiri anayefahamika kwa jina la Crixocrix na Nusder kutoka jijini Dar es salaam.

Akizungumzia kuhusu ujumbe ulio katika wimbo huu mzuri mwimbaji Fabrice J. Prince amesema:-

”AMANI ni hali ya salama iliyo ndani ya moyo wa mwanadamu, pasipo fujo wala ugomvi.. Na kukosekana kwa amani ya ndani ya moyo huharibu amani ya nje pia.. Wengi hawajui hii amani chanzo chake ni kipi naomba kila mtoto wa Mungu achukue nafasi ya kusikiliza wimbo huu kwa makini na nina hakika atapata jibu la Amani.. Nakukupa amani.. Asante, ukipata amani sambaza amani kwa wengine pia Mungu akubariki sana…” – Fabrice J. Prince.

Hakika hii ni moja kati ya kazi nzuri sana zilizofanyika mwaka 2017 ikiwa na kusudi la kufikisha ujumbe wa Mungu kwako mwana wa Mungu huku ukimsifu na kumfurahia kwa muziki mzuri ulioandaliwa kwa ustadi wa kiwango cha juu cha ubora katika kuhakikisha neno la Mungu linatangazwa kwa viwago vya kipekee.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakufanya uwe na amani ya moyo muda wote utakapokuwa unausikiliza wimbo huu na kutazama video hii. Mungu akubariki na kukupa amani ya moyo mwana wa Mungu.. Barikiwa!!

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Fabrice J. Prince kupitia:
Simu/WhatsApp: +14344651647
Facebook: Fabrice J Prince
Instagram: @official_fabricejprince
Twitter: @OfficalJfabi
Email: j.fabrice2016@gmail.com
YouTube: OfficialFabriceJ Prince

More in Video

FEATURED MUSIC

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

JIUNGE NASI

Jiunge na blog ya gospomedia.com ili uwe wa kwanza kupokea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kila siku kupitia barua pepe yako.

Join 13,131 other subscribers

Gospomedia.com ni blog rasmi inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kilasiku kutoka ndani na nje ya Afrika.

To Top