Connect with us

Video | Tanzania One Soul – Ni salama

Video

Video | Tanzania One Soul – Ni salama

Kwa masikitiko makubwa leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com tumekuwekea video ya wimbo wa maombolezo ya ajali ya wanafunzi waliopoteza maisha wakiwa kwenye basi huko mkoani arusha wimbo huu unaitwa Ni salama.

Video hii imeongozwa na director Einxer, Muziki ukiwa umeimbwa na baadhi ya waimbaji mahiri wa muziki wa Injili kutoka Tanzania (Tanzania One Soul) akiwemo Angel Benard, Miriam Jackson, Goodluck Gozbert, Miriam Lukindo, na Joel Luwaga ambao kwa pamoja wameomboleza msiba huu mzito kupitia wimbo maalumu wa majaonzi na salamu za rambirambi kwa wazazi, ndugu waliofikwa na msiba huu na taifa kwa ujumla.

Ikumbukwe kuwa msiba huu umehusisha wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent ambao walipata ajali ya basi iliyotokea katika korongo la mlima wa Rhotia, karatu, mkoani Arusha siku ya jumamosi ya tarehe 6.05.2017 ambapo imethibitishwa kuwa zaidi ya wanafunzi 25, walimu wawili na dereva mmoja wa basi la shule ya Lucky Vincent iliyopo jijini Arusha wamefariki dunia wakiwa ndani ya basi hilo ambalo lilipata ajali.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha uweze kutazama video hii ikiwa ni sehemu ya kuwafariji ndugu, jamaa na watanzania wote tulioguswa na msiba huu mzito.

Download

Uongozi na timu nzima ya gospomedia tunapenda kuchukua nafasi hii pia kutoa pole kwa wafiwa wote na taifa kwa ujumla, tunazidi kuwaombea kwa Mungu azidi kuwatia nguvu ya misuli ya imani katika kipindi hiki kigumu ambacho tunaamini Mungu atakwenda kuwasimamia, “Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe”.

Like Page yetu ya facebook > Gospo Media instagram: @gospomedia

To Top