Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Nanyori Raymond-Ng'ang'ania - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Nanyori Raymond-Ng’ang’ania

Video

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Nanyori Raymond-Ng’ang’ania

Kutoka Arusha Tanzania, leo kupitia tovuti ya gospomedia.com tunaitambulisha kwako video mpya inayoitwa Ng’ang’ania kutoka kwa muimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Nanyori Raymond.

Video ya wimbo huu imeongozwa director Nisher kutoka studio ya Nisher Entertainment na audio ikiwa imetengenezwa ndani ya studio ya Christina Shusho Record chini ya mikono ya producer James Mbili.

Akiongea na gospomedia.com muimbaji Nanyori Raymond amesema kuwa video ya wimbo huu ndio inayobeba jina la album yake mpya ya Ng’ang’ania ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo nane ikiwa kwenye mfumo wa Audio Cd na Dvd lakini ambayo siku chache zijazo ataiachia sokoni na kusambaa mahali pote ili iweze kumfikia kila mtu katika kulitangaza neno la Mungu kupitia kipawa chake cha Uimbaji.

Muimbaji Nanyori ameongeza kuwa video ya Ng’ang’ania ni ujio wake wa pili kwa mwaka 2017 baada ya ile ya kwanza inayoitwa Sitaogopa.

Muimbaji Nanyori Raymond amewasihi wadau na wapenzi wa muziki wa Injili Tanzania na Afrika mashariki wampokee na waendelee kumpa sapoti ili azidi kuleta kazi nzuri zaidi zitakazokuwa Baraka kwa kila atakayesikiliza na kutazama kazi zake.

gospomedia.com tunakukaribisha kuitazama video ya wimbo huu mpya uitwao Ng’ang’ania kutoka kwa muimbaji Nanyori Raymond pia unaweza kusikiliza na kupakua wimbo huu hapa chini kisha mpe sapoti yako kwa kuwashirikisha na wengine kwa kadri uwezavyo ili Baraka hizi ziweze kuwafikia watu wengi zaidi mahala pote duniani kupitia nyimbo za Injili na hakika Mungu atakubariki sana. Karibu!!

Download

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Nanyori Raymond kupitia
Simu/WhatsApp: +255 758 890 490
Facebook: Nanyori Raymondi
Instagram: @nanyorray
YouTube: Nanyori Raymond
Email: nanyoriray@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements

More in Video

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top