Download Music Video + Audio: New Jerusalem Brothers Feat Neema Sadock-Kuliko Jana Cover - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Download Music Video + Audio: New Jerusalem Brothers Feat Neema Sadock-Kuliko Jana Cover

Video

Download Music Video + Audio: New Jerusalem Brothers Feat Neema Sadock-Kuliko Jana Cover

Shalom Shalom! leo kupitia tovuti ya gospomedia.com tumekuwekea wimbo mpya kutoka kundi la vijana wa New Jerusalem Brothers video ya wimbo huu inaitwa Kuliko Jana wakiwa wamemshirikisha mwanadada anayefahamika kwa jina la Neema Sadock, wimbo ukiwa umetengenzwa na producer Vankuva kutoka studio ya HomeTown iliyopo Dar es salaam.

Wakiongea na gospomedia mmoja wa wana kundi hilo la New Jerusalem Brothers Clinton Onditi amesema kuwa wanamshukuru Mungu kwa kuikamilisha video hii ambayo wanaamini itakuwa baraka kwa kila atakayekuwa anaitazama na kuisikiliza kilasiku kutokana na uwezo wa kiuimbaji waliotumia katika wimbo huu ijapokuwa wamepitia changamoto kadhaa katika kuikamilisha kazi hii lakini bado wanaamini watafika mahali pazuri zaidi kihuduma.

Pia wanatoa shukrani na heshima kwa kundi zima la Sauti Soul kutoka nchini kenya ambao ndio waliutoa wimbo huu kwa mara ya kwanza na wao wakaamua kufanya kwa uwezo wao kupitia wimbo huo na mahadhi yaliyofanyika kwenye wimbo wao.

Kundi hili la New Jerusalem Brothers limeundwa na vijana sita ambao ni Clinton Onditi, Francis bisanda, Elia Mchomvu, Erasto Chacha, Jacob Silas na Francis Richard.

gospomedia.com tunakukaribisha kuitazama video hii, kupakua na kusikiliza wimbo huu wa Kuliko Jana kisha uwashirikishe na wengine kwa kadri uwezavyo ili kuwapa sapoti vijana hawa kutoka kundi la New Jerusalem Brothers ili wengine waweze kubarikiwa pia kupitia wimbo huu na hakika Mungu atakubariki sana. Karibu!!

DOWNLOAD

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na kundi la New Jerusalem Brothers kupitia
Simu/WhatsApp: +255757830451 au +255657184087
Facebook: New J Brothers
Instagram: newjerusalembrotherstz
YouTube: Officialnewjerusalembrotherstz
Email: newjerusalebrotherstz@gmail.com

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram > @gospomedia

Advertisements

More in Video

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top