Download Music Video + Audio: Nanyori RayMond-Sitaogopa - Gospo Media
Advertisements
Connect with us

Gospo Media

Download Music Video + Audio: Nanyori RayMond-Sitaogopa

Video

Download Music Video + Audio: Nanyori RayMond-Sitaogopa

Kutoka Arusha Tanzania, leo kupitia tovuti ya gospomedia.com tunaitambulisha kwako video mpya inayoitwa Sitaogopa kutoka kwa muimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Nanyori Raymond.

Video ya wimbo huu imeongozwa director Nisher kutoka studio ya Nisher Entertainment na audio ikiwa imetengenezwa ndani ya studio ya Christina Shusho Record chini ya mikono ya producer James Mbili.

Akiongea na gospomedia.com muimbaji Nanyori Raymond amesema kuwa video ya wimbo ni moja kati ya video zinazopatikana kwenye album yake mpya inayobeba jina la Ng’ang’ania ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo nane ikiwa kwenye mfumo wa Audio Cd na Dvd lakini bado hajaiachia sokoni.

Muimbaji Nanyori ameongeza kuwa video ya Sitaogopa ni mwanzo wa ujio wake huu mpya kwa mwaka 2017 katika kumtumikia Mungu kupitia nyimbo za Injili hivyo amewasihi wadau na wapenzi wa muziki wa Injili Tanzania na Afrika mashariki wampokee na waendelee kumpa sapoti ili azidi kuleta kazi nzuri zitakazokuwa Baraka kwa kila atakayesikiliza na kutazama video atakazokuwa anaendelea kuziachia kwa uwezo Mungu.

gospomedia.com tunakukaribisha kuitazama video ya wimbo huu mpya uitwao Sitaogopa kutoka kwa muimbaji Nanyori Raymond pia unaweza kusikiliza na kupakua wimbo huu hapa chini kisha mpe sapoti yako kwa kuwashirikisha na wengine kwa kadri uwezavyo ili Baraka hizi ziweze kuwafikia watu wengi zaidi mahala pote duniani kupitia nyimbo za Injili na hakika Mungu atakubariki sana. Karibu!

Download

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Nanyori Raymond kupitia
Simu/WhatsApp: +255 758 890 490
Facebook: Nanyori Raymondi
Instagram: @nanyorray
YouTube: Nanyori Raymond
Email: nanyoriray@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements

More in Video

FEATURED MUSIC

Advertisements

TOP 5 ON GOSPOMEDIA.COM

Gospomedia.com ni blog ya kikristo inayokuletea nyimbo na video mpya za muziki wa Injili.

To Top