Burudani

Wewe Ni Neema Ni Ujio Mpya wa Mwimbaji Theofrida Gervas.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka jijini Dar es salaam Tanzania  Theofrida Gervas ameweka wazi ujio wa video yake mpya iitwayo Wewe ni Neema ikiwa ni video yake ya pili baada ya video yake ya kwanza aliyoiachia mwishoni mwa mwaka 2016 inayofahamika kwa jina la Jesus.

Akiongea na timu ya habari ya gospomedia mwimbaji Theofrida Gervas amesema ”Baada ya ukimya wa muda mrefu nikiwa katika maandalizi ya kukamilisha videos za album yangu ya Mshukuruni Bwana napenda kuwafahamisha wapenzi na wadau wa muziki wa Injili kuwa kwa Neema ya Mungu nitaachilia video yangu mpya iitwayo ”Wewe Ni Neema” ikiwa ni moja kati ya nyimbo zilizo kwenye album yangu ya ”Mshukuruni Bwana” Hivyo nawaomba mashabiki na wadau wote wanaopenda na kufuatilia muziki wa Injili hapa kwetu Tanzania kuipokea taarifa hii kwa furaha kwa maana kupitia ujio wangu huu mpya watapokea baraka na kuinuliwa katika viwango vingine vya kiroho.

Mwimbaji Theofrida Gervas amesisitiza pia juu ya ujio wa album yake ya video DVD ya MSHUKURUNI BWANA ambayo ipo mbioni kukamilika na itaingia sokoni baada ya ukamilifu wake.

Kama bado hujaitazama video ya JESUS kutoka kwa mwimbaji Theofrida Gervas kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kuitazama na kuupakua wimbo huu hapa na hakika utabarikiwa. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Theofrida Gervas kupitia
Simu/WhatsApp: +255655 605 377
Facebook: Theofrida Gervas Vena
Instagram: theofridagervas70
YouTube: theofrida gervas

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Tazama Video | Download Audio: Peter Mdoe - Mpaji Mungu

Next post

Uchaguzi Mkuu CHAMUITA kufanyika Tarehe 29 Septemba 2017.