Habari

Watu 26 wameuwawa kwa kupigwa risasi katika kanisa la First Baptist, Texas.

Texas, Marekani.

Watu 26 wameuwa na wengi zaidi wamejeruhiwa baada ya kupigwa risasi katika kanisa la First Baptist Church lililopo mjini Texas siku ya Jumapili, Novemba 5.

Kwa mujibu wa Habari za CBN zinasema kuwa, mtuhumiwa aliingia katika kanisa la First Baptist huko Sutherland Springs, Texas muda wa saa 11:20 asubuhi na kuanza kufyatua risasi kwa watu wote waliokusanyika kwenye ibada ya Jumapili hiyo.

Waathirikawa wa shambulio hilo ni pamoja na watoto na wazee waliokuwa kwenye ibada hiyo na imethibitishwa kuwa Mchungaji wa kanisa hilo, Frank Pomeroy, amempoteza binti yake aliyekuwa na umri wa miaka 14.

Polisi wameshamtambua mtuhumiwa wa shambulio hilo kuwa ni Devin Kelley mwenye umri wa miaka 26. Kelley aliripotiwa kuwa alikimbilia kanisani mara baada ya mkazi mmoja wa eneo hilo kujaribu kupambana naye. Alikutwa amekufa katika gari lake mara baada ya kukwama wakati akijaribu kukimbia huku mwili wake ukiwa na jeraha la risasi , ingawa bado haijatambulika wazi kama jeraha hilo lilijitokeza kabla au lilijitokeza wakati akiwa anafukuzana na polisi.

Viongozi wa usalama wamesema kuwa kwasasa wanaishughulikia kesi hiyo na kutambua taarifa zote zinazomhusu mtuhumiwa juu ya shambulio hilo kwakuwa mpaka sasa, hawana ushahidi wowote kwamba Kelley alikuwa ana uhusiano au kushirikiana na shirika lolote la kigaidi.

Kufuatia mkasa wa shambulio hilo, Meya wa jimbo la Texas Greg Abbott alikuwa na haya ya kusema katika mkutano wa waandishi wa habari, “Kuna maisha ya watu 26 ambayo yamepotea. Hatujui kuwa watu hao watafufuka au la, Ingawa wote tunafahamu kuwa idadi hii ni kubwa sana, na haya yatakuwa ni maumivu ya muda mrefu na kuteseka hasa kwa wale walio katika na maumivu haya. Tunaomba faraja ya Mungu, mwongozo wa Mungu na kwa uponyaji wa Mungu kwa wale wote wanaoteseka. Nikiwa kama gavana, ninaomba kila mama na baba mkiwa nyumbani usiku wa leo, weka mikono yako kwa mtoto wako na kukumbatia kwa upendo na mfanye ajue kuwa ni kwa jinsi gani unampenda na kujua kwamba sote tunasaidiana. ”

Rais Trump pia alitoa maoni juu ya shambulio la risasi akiwa nchini Japan na kuamua kusitisasha ziara yake ya barani Asia:

“Mawazo yetu na sala zetu ni pamoja na waathirika na familia katika mashambulizi ya leo ya kutisha,” Trump alisema. “limetokea mahali pa ibada takatifu. Maumivu na huzuni tunayohisi siwezi kuanza kufikiria mateso ya wale waliopoteza wapendwa wao.”

“Katika kipindi cha majanga wamarekani tutafanya kile tunachofanya vyema zaidi: tunaungana pamoja na kushikana mikono na kupitia machozi na huzuni tunasimama Imara,” aliongeza.

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Hizi ndizo nyimbo kumi bora zilizofanya vizuri mwezi septemba 2017.

Next post

Video Music | Audio Music: Paul Clement - Namba Moja