Video

Tazama Video Music | Download Audio: Edwin Mrope – Mponyaji

Dar es salaam,

Shalom mwana wa Mungu! leo nimekuletea video iitwayo Mponyaji kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa Singeli anayefahamika kwa jina la Edwin Mrope.  Video ya wimbo huu imeongozwa na director Fahim Rasham na wimbo ukiwa umetengenezwa na Edwin Mrope akiwa ndiye prodyuza wa wimbo huu.

Mponyaji ni wimbo wa Sifa unaozungumzia Uponyaji wetu sisi kama wana wa Mungu ambao uhai wetu unamtegemea Yesu Kristo ambaye kwa upendo wake aliamua kufa msalabani ili sisi tupone na kuwa wapya, katika wimbo huu mtumishi Edwin Mrope amezungumzia matukio mengi ambayo ni ushuhuda juu ya matendo aliyoyafanya Yesu Kristo kwa watu mbalimbali akiwemo Batholomeo(Bartholomew) ambaye aliweza kupokea uponyaji baada ya kuwa kipofu kwa muda mrefu, wimbo huu unakupa moyo hata wewe unayepitia hali ya magonjwa, kukataliwa na hata kukutana na vikwazo vya kila aina usikate tamaa bali mpokee Yesu Kristo na hakika atakwenda kutenda jambo kuu la uponyaji juu ya maisha yako leo.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kuitazama video hii na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma  wasiliana na mwimbaji Edwin Mrope kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 713 246 084
Facebook: Edwin Mrope
Instagram: @edwinmrope

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Elly Joh: Tarehe 8 Oct 2017 ndio siku pekee Nitakayoachia pumzi yangu rasmi

Next post

Tazama Video | Download Audio Music: AD Music - Kimbilio