Videos

Tazama Video | Download Official Audio: Preye Odede – I am Real

Video iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa sana iitwayo ”I AM REAL” kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini nigeria Preye Odede sasa imeachiwa rasmi.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Preye alifanikiwa kujipatia umaarufu mkubwa kupitia wimbo wake wa kusifu na kuadubu uitwao “Ebezina” na kupata mafanikio makubwa ya kimuziki mara baada ya kuachia albamu yake ya kwanza iitwayo ”My Script” na kuachia nyimbo kadhaa kutoka kweye album hiyo ikiwemo ”Bulie”, ”Hossana”, na ”No Other God” ukiwa ni wimbo ambao aliuachia hivi karibuni kutoka kwenye albamu hiyo.

Hivi karibuni dada yake alifanyiwa upasuaji iliopelekea kupata matatizo makubwa ya kiafya licha ya Preye kuomba sana msaada wa maombi kutoka kwa marafiki zake na wafanyakazi wenzake lakini Mungu aliweka moyoni mwake wimbo mpya uitwao ”I’am Real” (Mimi ni Halisi) usiweke macho yako mbali nami” na wakati akiendelea kuabudu nguvu ya Mungu ilijidhihirisha wazi na leo dada yake ni mzima kiafya.

Huu ni wimbo kutoka kwenye album yake ya pili inayobeba jina la “Ready” anayotarajia kuiachia hivi karibuni.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao utafanyika baraka katika maisha yako kwakuwa Mungu ni Halisi . Karibu na ubarikiwe!!

Download Audio

Wasiliana na mwimbaji kupitia kupitia:

Twitter @PreyeOdede
Instagram @preyeodede
Website : http://www.preyeodede.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Mwimbaji James Nyambega Atamani Kufanya Colabo na Witness Mbise.

Next post

Video | Download Music Audio: Meshack Alphonce - Sema Nao