Video

Tazama Video | Download Music Audio: Neema Ng’asha – Usilie Tena

Kutoka Dar es salaam Tanzania, leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com tumekuwekea video mpya kutoka kwa muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Neema Ng’asha video hii inaitwa Usilie Tena ikiwa imeongozwa na studio ya Mwamakula Production na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio ya Apao Records chini ya mikono ya producer Issam.

Akiongea na timu ya wanahabari wa gospomedia.com muimbaji Neema Ng’asha ameongeza kuwa video hii ndio inayobeba jina la albamu yake mpya inayofahamika kwa jina la ” Usilie Tena “ ambayo itapatikana kwenye mfumo wa video DVD na Audio CD ambayo ipo mbioni kuingia sokoni muda wowote kuanzia sasa na anaamini kupitia video hii mpya watu watu wengi watakwenda kufunguliwa na kuinuliwa upya katika maisha yao licha ya changamoto walizonazo hivyo amewataka wapenzi wote wa nyimbo za Injili na wadau mbalimbali kutoka pande zote za nchi na dunia kwa ujumla kumpa sapoti ya kuusambaza ujumbe ulio katika wimbo na video hii ya Usilie Tena kwakuwa anaamini kuwa watu wengi watabarikiwa.

gospomedia.com inakukaribisha kuitazama video hii na kupakua wimbo huu iliyojaa ujumbe wenye baraka kwako na hakika ubarikiwa sana.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Neema Ng’asha kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 673 527 249
Facebook: Neema Ng’asha
Instagram: @neema.ngasha
Blog: www.neemangasha.blogspot.com

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Onstage: Mwimbaji Joseph Mabula akiimba wimbo wake wa Chuki ya Nini ktk kanisa la ELOI,Kigamboni.

Next post

Download Music Audio: Walter Chilambo - Namba Moja