Music

Tazama Video | Download Music Audio: Deborah Mkonya – Kwa Nguvu za Mungu

Deborah Mkonya ni muimbaji mpya wa nyimbo za Injili aliyebarikiwa sauti nzuri kutoka jijini Dar es salaam na leo kupitia blog yako pendwa anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya iitwayo Kwa Nguvu za Mungu ikiwa imeongozwa na director Yotham Lyobha na wimbo ukiwa umtaayarishwa na prodyuza Innocent Mujwahuki kutoka Push Up Entertainment.

Debora Mkonya mwanachama wa timu ya kusifu na kuabudu kutoka kanisa la Chuo cha Manabii chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Maboya.

“Kwa nguvu za Mungu ” ni nyimbo ya kwanza kabisa kutoka katika albamu yake ya kwanza iitwayo “Neema”, ikiwa na mkusanyiko wa nyimbo nane na yote ikiwa imefanyika studio za Push up Entertainment na inatarajiwa kutoka Januari 26, 2018.

Katika video hii muimbaji Deborah amezungumzia juu ya Nguvu za Mungu jinsi zinavyotenda miujiza juu ya maisha yake na hata kwa maisha ya watu wengine na kusisitiza watu juu ya kuamini katika Mungu wa kweli kwakuwa ushindi wetu upo kwa yeyote aaminiye katika Nguvu za Mungu, Ni pale tu mwana wa Mungu atakapojitambua kuwa yeye ni nani na nani aliye ndani yake kiuhalisia kabisa anakuwa ameshayapata majawabu ya mahitaji yake.

gospomedia.com tunakupa nafasi ya kuitazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao hakika utakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Deborah Mkonya kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 653 520 088/+255 764 608 236
Facebook: Deborah Mkonya
Instagram: @deborahmkonya
E-mail: deborahmkonya06@gmail.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Download Audio: Dorcas Japhet - Nakupa Moyo

Next post

Download Music Audio: Dr.Tumaini Msowoya - Furaha