Video

Tazama Video | Download Audio: Peter Mdoe – Mpaji Mungu

Shalom mwana wa Mungu! leo kwa mara nyingine tumekusogezea video mpya itwayo Mpaji Mungu kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Peter Mdoe, video ikiwa imeongozwa na director Clevor na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Republic of Music chini ya mikono ya prodyuza Mpeula.

Hii ni moja ya kazi zenye nguvu kubwa ya baraka ya kukutia moyo na kukuinua hasa kwa wewe mwenye kukata tamaa kutokana na mapito magumu unayopitia. Kupitia video hii mwimbaji Peter Mdoe anatukumbusha kuwa kuna nafasi ya Mungu katika maisha yetu ambayo unapaswa kuitafuta ili ukuu wake uweze kuonekana nguvu ya Mungu ni kubwa sana tofauti na binadamu wafikiriavyo pindi tupatapo majaribu na vikwazo vya kila aina.

kupitia wimbo huu mwimbaji Peter Mdoe anatusisitiza kuwa dawa ya matatizo yetu ni Mungu pekee kupitia mwanae Yesu Kristo ambaye anatupatia kibali cha ukombozi katika maisha yetu na kutengwa mbali na uovu wa shetani, hakika hii ni moja kati ya nyimbo zenye nguvu ya baraka pindi unapoisikiliza na kweli utabarikiwa.

Kwa moyo wa unyenyekevu tunakukaribisha kutazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu wenye baraka ya kukutia Moyo na kukuinua. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Peter Mdoe kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 655 094 891
Facebook: Peter Mdoe
Instagram: @peter_mdoe

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Audio: Joel Lwaga - Pendo

Next post

Wewe Ni Neema Ni Ujio Mpya wa Mwimbaji Theofrida Gervas.