Videos

Tazama Video | Download Audio: Mr.Mike & Hype Burton – Nakupenda

Kutoka mjini morogoro mpaka Dar es salaam Tanzania leo tumekusogezea video mpya iitwayo Nakupenda kutoka kwa muimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Mr.Mike akiwa amemshirikisha Hype Burton.

Video hii imeongozwa na kampuni ya Revolution Entertainment na wimbo ukiwa umetaayarishwa na prodyuza Sulesh kutoka mjini morogoro.

Huu ni wimbo wa kusifu ambapo mwimbaji Mike anatukumbusha kumpenda Mungu kupitia manaye Yesu Kristo kwakuwa yeye ni Baba yetu aliyetuumba kwa mfano wake na ndiye mkuu anayetawala duniani na mbinguni, hivyo ndivyo wana wa Mungu wanatakiwa kumtukuza Mungu kwa mambo yake makuu ambayo anaendelea kututendea hadi leo.

kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu kutazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utaachilia baraka juu yako. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Mr.Mike kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 717 589 151
Facebook: Mr mike Tz
Instagram: @mr_mike_tz

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Download Music Audio: Xcel Siri - Flourishing

Next post

Kitabu cha Mwanamke wa Agano Sasa Kinapatikana Madukani Rasmi.