Video

Tazama Video | Download Audio: Milca Kakete – Siku Imeanza

Kutoka nchini canada mpaka Tanzania, leo tumekusogezea video ya wimbo mpya uitwao Siku Imeanza ikiwa ikiwa imeongozwa na director Alex Joseck kutoka studio za Enzi Films.
Video hii inapatikana kwenye album yake mpya iitwayo Siku Imeanza ikiwa ndio wimbo pekee iliyobeba jina la album hiyo ambayo alifanikiwa kuizindua mwezi wa nne mwaka huu wa 2017 huko nchini canada.
 
Akiongea na gospomedia muimbaji na mtumishi wa Mungu Milca Kakete amesema kuwa album yake hii mpya ni yenye mkusanyiko wa nyimbo zenye baraka na za kuinua mioyo ya watu wote bila kujali dini, rangi wala madhehebu yao hivyo amewasisitiza wapenzi na wadau wote wa kazi za Milca Kakete na muziki wa injili kwa ujumla kumuunga mkono katika kuinunua albamu yake hii mpya ambayo anaamini itawabariki wengi mno.
Kwa moyo mkunjufu gospomedia.com tunakukaribisha kutazama, kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao hakika utakubariki kila utakapokuwa unausikiliza. Karibu!!

Kwa mawasiliano zaidi juu ya kupata album hii na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Milca Kakete kupitia
Simu/WhatsApp: +1(905) 341 56 64
Facebook: Milca Kakete
Instagram: @milcakakete
Twitter: milca kakete
Facebook Page: Milca Kakete Ministry
Email: milcakakete@yahoo.com

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Audio: Shadrack Ngailah - Macho Ya Roho

Next post

Tazama Video | Download Audio: Christina Shusho - Roho