Video

Tazama Video | Download Audio: Lillian Mc Jairo Feat Sylvia Akoth – Baraka

Shalom mtu wa Mungu, leo kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tumekusogezea video mpya iitwayo Baraka kutoka kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Kenya aayefahamika kwa jina la Lilian Mc Jairo akiwa amemshirkisha mwimbaji anayefahamika kwa jina la Sylivia Akoth, video ikiwa imeongozwa na director M-Kisavi kutoka studio za Touch of a KinG na wimbo ukiwa umetaayarishwa na prodyuza anayefahamika kwa jina la Esynet.

Wimbo huu unaelezea nguvu ya Baraka ambazo hutolewa na Mungu pekee kwa yeyote anayeamini na aliyeamua kumpa Yesu Kristo maisha yake na kumtumikia vile inavyopasa na kumfanya kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake, Huu ni ujumbe wa pekee kutoka kwa mtumishi Lilian Mc Jairo akitukumbusha kuwa kumtegemea Mungu kuna faida kubwa katika kufungua milango ya Baraka ambazo zinabadilisha maisha yetu kutoka chini kweda juu zaidi na kukata minyororo yote ya vifungo vya adui shetani.

Kwa moyo mkunjufu tuakukaribisha utazame video hii nzuri, usikilize na kupakua wimbo huu na hakika wimbo huu utakuwa ni sehemu ya Baraka katika maisha yako kama utaaamini na kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Lillian Mc Jairo kupitia
Simu/WhatsApp: +254 723 536 031
Facebook: Lillian M’c Jairo
Instagram: @lilyjairo

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Julius Julius Mgundoy Aweka Wazi Miango Yake Kuelekea 2018.

Next post

Download Audio: Badimo Elias - Gitaa Langu