Videos

Tazama Video | Download Audio: Lecrae feat. Tori Kelly – I’ll Find You

Kutoka nchini marekani leo tumekusogezea video mpya iitwayo ‘I’ll Find You’ kutoka rapa mahiri wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina Lecrae akiwa amemshirikisha mwanadada Tori Kelly.

Video hii imebeba ujumbe wa  matumaini na faraja kwa wagonjwa wote hasa wa saratani ambao kupitia video hii inaonyesha watoto wadogo wakiwa ni wagonjwa wa saratani wakiwa wamejazwa uhai katika ulimwengu wa roho huku wakisaidiana kurudisha afya zao, huku kwenye ulimwengu wa mwili wakionekana ni wadhaifu wanaohitaji msaada wa kimwili kama vile matibabu, chakula mavazi n.k hii inatoa ujumbe wa picha wa kuwakumbusha na kuwahamasisha watu kuwa na moyo wa upendo na wa kujitolea kwa wanaohitaji msaada wetu kama vile wagonjwa n.k na hapo ndipo upendo wa Mungu utadhihirika juu yetu.

Mwisho wa video hii inaonyesha baadhi ya watoto wachache walioathirika na ugonjwa wa saratani ikiwa na pamoja na link maalumu ya kuchangia ili kuwasaidia wagonjwa hao wa saratani katika hospitali ya saratani ya St. Jude’s.

gospomedia.com tunakukaribisha kuitazama video hii kwa makini na kupakua wimbo huu ambao hakika utakuwa baraka sana kwako siku ya leo na Mungu akubariki.

Download Audio

Social Media

Facebook: Lecrae
Instagram: @lecrae
Twitter: @lecrae
Website: www.lecrae.com

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Download Audio: Otor Clement - Thank You Lord

Next post

Tazama Video | Download Music Audio: T.S Itopa Feat Johnny K. Palmer - Unrestrained