Videos

Tazama Video | Download Audio: Judia Amisi – Ni Neema

Kutoka jijini Dar es salaam tumekusogezea video mpya iitwayo Ni Neema kutoka kwa mwimbaji anayefahamika kwa jina la Judia Amisi, video hii imeongozwa na studio ya Still Alive na wimbo ukiwa umefanyika pia ndani ya studio ya Still Alive.

Ni Neema ni wimbo uliobeba ujumbe wa Ki-Mungu kupitia mwimbaji Judia ambaye ameeleza vyema juu ya nguvu ya Neema ambayo wengi tumekuwa tukishindwa kuitumia vyema kutokana na kutokufahamu ni kwa jinsi gani Mungu amekuwa akitubariki kupitia vitu na mambo mbalimbali mazuri ambayo yanatokana na Neema ambayo Mungu anaiachilia kwenye maisha yetu na sasa kupitia wimbo huu anatukumbusha na kutoa neno la matumaini juu ya Nguvu ya Neema inavyotenda kazi kubwa katika maisha yetu kwa maana hata uhai, vipawa na vyote tulivyonavyo ni kwasababu umepewa Neema hivyo huna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo ili aendelee kukutumia kama chombo cha baraka kwa wengine wenye kuhitaji.

Huu ni wimbo wa kubariki na kuinua sana kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu ambao tuna hakika utakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Judia kupitia
Facebook: Judia Amisi
Instagram: @judia9
Snapchat: Judia99

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Download Audio: Chris Shalom - Your Word Is Truth

Next post

Tamasha kubwa la Nuru ya Mtaa Kufanyika Tarehe 17.09.2017 Jijini Arusha.