Video

Tazama Video | Download Audio: Jimmy Gospian – Nimekuona

Shalom mwana wa Mungu! leo kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tumekusogezea video mpya kabisa iitwayo Nimekuona kutoka kwa mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza na huyu si mwingine bali ni Jimmy Gospian video ikiwa imeongozwa na director Kenny Ukiyz na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Vibe Nation chini ya usimamizi wa prodyuza Nusder kutoka jijini Mwanza.

Nimekuona ni wimbo wa kumtukuza Mungu ukiwa unadhihirisha utii na unyenyekevu wa kumtumikia Mungu katika roho na kweli kama mwimbaji Jimmy Gospian anavyotukumbusha kupitia wimbo huu na video hii kuwa Mungu ndio kimbilio letu na hivyo kila mwenye pumzi na amsifu Bwana kwakuwa Baraka na Neema zote zinatoka kwake na zaidi ya yote tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo ambalo anatutendea katika maisha yetu kwakuwa si kwa nguvu zetu bali ni kwa nguvu za Mungu mkuu juu yetu. Yoh 6:46

Hakika huu ni moja kati wimbo wenye kutia nguvu na baraka sana unapousikiliza na kutazama video hii ambayo imeandaliwa kwa kiwango bora sana na imedhihirisha wazi kuwa Mungu wetu ni wa viwango vya juu. Halleluya!!

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakwenda kubadilisha maisha yako na kukubariki siku zote. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Jimmy Gospian kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 759 950 978
Facebook: Jimmy Gospian
Instagram: @jimmygospian

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tamasha la Mwanamke wa Imani Kufanyika Septemba 17, 2017 Kigamboni.

Next post

Download Audio: Annukka Neema Mwaikuju - Mungu wa Israel