Video

Tazama Video | Download Audio: Ephy Young – Niko Sawa

Kutoka nchini Kenya leo tumekusogezea video ya wimbo uitwao Niko Sawa kutoka kwa mwimbaji mwenye umri mdogo katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Kenya anayefahamika kwa jina la Ephy Young video ikiwa imeongozwa na Trued Pictures na wimbo ukiwa umetayaarishwa na prodyuza Teddy B akishirikiana na Pitson na Paper.

Wimbo huu unaelezea Sifa na shukrani kwa Mungu kwa yale mwimbaji Ephy Young ametendewa maishani mwake na sasa kupitia wimbo huu anakiri kuwa Yesu kwake ni Bwana na mwokozi wa maisha yake na anajisihi yupo sawa akiwa naye maana kwake hakuna linaloshindikana.  Hii ni moja kati ya kazi zake zinazofanya vizuri sana kwenye vituo mbalimbali vya radio na televisheni ndani na nje ya Kenya.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakuwa ni baraka kwako.

Download Audio

Wasiliana na mwimbaji Ephy Young kupitia:

Facebook Page: Ephy Young
Instagram: @ephyyoung

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Audio: Pompi - Silence

Next post

TAMUFO na NSSF kuwawezesha wanamuziki kiuchumi septemba 2, 2017.