Video

Tazama Video | Audio Music: Alphee Niyo – Songa Mbele

Kutoka nchini marekani mpaka Tanzania leo kwa utukufu wa Mungu nimekuletea wimbo uitwao ”Songa Mbele” kutoka kwa mtumishi wa Mungu anayefahamika kwa jina la Alphee Niyo, video hii imeongozwa na studio za Still Alive na audio ikiwa imetayaarishwa ndani ya studio za Still Alive zilizopo nchini kenya.

Songa Mbele ni wimbo uliobeba kusudi la kuwapa watu nguvu ya matumaini mapya ili kuweza kusonga mbele kwakuwa Mungu anakusudi la kutupitisha mahali penye ushuhuda wa pekee wenye kumtukuza na kumsifu yeye siku zote.

Haijalishi ni mapito magumu kwa kiasi gani tunapitia katika maisha yetu jambo moja unalopaswa kujua ni kusonga mbele usirudi nyuma na Mungu atakupigania na mwisho utakuwa shujaa.

Alphee Niyo ni mwimbaji mwenye asili ya Tanzania ambaye kwasasa anaishi nchini marekani na wimbo huu wa Songa Mbele ndio wimbo unaobeba jina la albamu yake mpya iliyo katika mfumo wa Audio CD na sasa ikiwa inapatikana madukani na unaweza kupiga namba hii +255 655 386 260 na utaletewa mahali popote ulipo.

Kwa moyo wa unyenyekevu nakukaribisha kutazama na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana siku ya leo. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Alphee Niyo kupitia:
Simu/WhatsApp: +18593821730

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Audio Music: Paul John - Yesu Asali

Next post

Tazama Video | Download Music: Lydia Livingstone - Chineke