Videos

Tazama Official Video | Download Music Audio: Emma – Nachotaka

Kutoka jijini Nairobi nchini Kenya tumekusogezea video mpya na yenye baraka iitwayo Nachotaka kutoka kwa mwimbaji mwenye sauti iliyojaa mafuta ya upako anayefahamika kwa jina la Emma Omongi, video hii imeongozwa na Director GadGado kutoka studio ya Reyo Films International na audio ikiwa imetayaarishwa na prodyuza mahiri anayefahamika kwa jina la Noel Waitara kutoka nchini kenya.

Huu ni wimbo wa kipekee sana kwa jinsi ambavyo mwimbaji Emma ametumia kipawa chake katika kutuletea ujumbe wa Mungu kupitia muziki huu na hakika kazi hii itakuwa ni ya baraka mno kwako mwana wa Mungu.

Katika wimbo huu mwimbaji Emma ameweka wazi hisia zake za ndani kabisa juu ya uhitaji wa moyo na roho yake kuwa karibu na upendo wa Yesu Kristo ambaye hana kipimo wala kikomo cha kutupenda na kutulinda, hakika huu ni wimbo utakaokuweka karibu zaidi na Mungu pindi utakapokuwa unatazama video hii na kusikiliza wimbo huu na hakika utakiri kuwa roho na mwili wako umepokea utakaso mpya kupitia jina la Yesu Kristo.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kutazama video hii na kupakua wimbo huu wenye mafuta ya upako ambayo yatakwenda kubadilisha maisha yako na kubarikiwa kwenda juu zaidi. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Emma Omongi kupitia:
Whatsapp: +254 722 663 710
Facebook page: Emma omonge Live
Instagram: official_emmamusic
Youtube: EmmaLiveTube

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Tazama Video | Download Music Audio: Rachael Owojori - Let’s Praise Him

Next post

Download Audio: Yared Ndolosi - Mshukuruni Bwana