Gospomedia.com ni tovuti rasmi kutoka Tanzania ambayo hukuletea habari za kikristo, mafundisho, mahubiri, matangazo, matukio, nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Mpaka sasa tovuti hii imekuwa na mafanikio makubwa tangu ilipoanzishwa mwaka mmoja uliopita na kuweza kuifikia jamii kubwa ya wakristo kutoka ndani na nje ya Tanzania, ambapo kila siku tovuti hii imekuwa inatembelewa mara zaidi ya laki mbili kutoka nchi zaidi ya hamsini duniani kote ikiwemo Tanzania, Kenya, Marekani, Uingereza, Afrika Kusini, Nigeria n.k

Tovuti hii pia imekuwa inatembelea wa watu wa jinsia zote na rika kuanzia miaka 18 na kuendelea na kufanya kuwa chombo pekee kinachoifikia jamii hasa ya wakristo katika kuwapa habari za kikristo, mafundisho, nyimbo na video mpya za muziki wa Injili kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa njia ya mtandao.

Gospo Media inayofuraha kukaribisha Taasisi, makanisa, mashirika, makampuni, wafanyabiashara, shule, vyuo na watu binafsi kutangaza kupitia tovuti ya gospomedia.com na kuifikia jamii hii kwa upana na kwa viwango vya bei nafuu.

Kwa huduma ya kuweka matangazo kwenye tovuti ya gospomedia.com tafadhali wasiliana nasi kupitia simu +255 755 038 159 au tutumie barua pepe kupitia gospomedia@gmail.com