Music

Sikiliza & Download Music Audio: Machalii Wa Yesu – Faraja Yako

Kwa masikitiko makubwa leo kupitia tovuti yako pendwa ya gospomedia.com tumekuwekea wimbo wa maombolezo ya ajali ya wanafunzi waliopoteza maisha wakiwa kwenye basi huko mkoani arusha wimbo huu unaitwa Faraja Yako kutoka kwa kundi la waimbaji wa nyimbo za Injili kwa mtindo wa HipHop linalofahamika kwa jina la Machalii wa Yesu kutoka Arusha.

Ikumbukwe kuwa msiba huu umehusisha wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent ambao walipata ajali ya basi iliyotokea katika korongo la mlima wa Rhotia, karatu, mkoani Arusha siku ya jumamosi ya tarehe 6.05.2017 ambapo imethibitishwa kuwa zaidi ya wanafunzi 25, walimu wawili na dereva mmoja wa basi la shule ya Lucky Vincent iliyopo jijini Arusha wamefariki dunia wakiwa ndani ya basi hilo ambalo lilipata ajali.

gospomedia.com tunakukaribisha uweze kutazama video hii, kusikiliza na kupakua wimbo huu wa majonzi na salamu za rambirambi kwa wafiwa wote ambao wamefikwa na msiba huu mzito.

Download

Uongozi na timu nzima ya gospomedia tunapenda kuchukua nafasi hii pia kutoa pole kwa wafiwa wote na taifa kwa ujumla, tunazidi kuwaombea kwa Mungu azidi kuwatia nguvu ya misuli ya imani katika kipindi hiki kigumu ambacho tunaamini Mungu atakwenda kuwasimamia, “Bwana Ametoa Bwana Ametwaa Jina lake lihimidiwe”.

Like Page yetu ya facebook > GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Comments

comments

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa watu na taasisi mbalimbali ambazo hutumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Sikiliza & Download Music Audio: Black Samaritan Feat Lunger, Stella & Solver-Ahadi

Next post

Tazama Video | Sikiliza & Download Music Audio: Pastor Mwambona Feat Ashley Nassary - Mwamba