Habari

SABA WAOKOKA KWENYE USIKU WA GOSPEL HIP HOP, WENGI WAFUNGULIWA KWENYE VIFUNGO.

Watu takribani saba wameamua kumpa Yesu maisha yao siku ya tamasha kubwa la muziki wa injili lililokwenda kwa jina la Usiku wa gospel Hip hop lililofanyika kwenye kanisa la T.A.G DMC tabata Segerea Chama kwa Mchungaji Dr. BonVenture Katembo likiongozwa na wanaharakati wa Yesu Okoa Mitaa.

waongofuu

Watumishi wa Mungu wakiombea watu waliompa Yesu maisha yao kwenye usiku wa gospel hip hop

Baada ya waimbaji kadhaa kuhubiri kwa njia uimbaji wa Rap kwenye tamasha hilo lilioanza saa tatu usiku alisimama mwenyekiti wa Yesu Okoa MitaaRungu la Yesu kutoa nasaha na ushuda mfupi kuhusu maisha yake na kisha kualika watu waliotaka kumpa Yesu maisha yao ambapo waliongozwa na sala ya toba kutoka kwa mchungaji wa kanisa hilo Dr. BonVenture Katembo. Katika hatua nyingine watu kadhaa walifunguliwa kutoka kwenye vifungo mbalimbali ikiwemo uvimbe tumboni, kuziba kwa mirija ya uzazi na ndoto mbaya baada ya maombi yaliyoongozwa na Mchungaji Laiza wa huduma ya GKM kwenye mkesha huo ambapo mchungaji aliwaagiza baadhi ya watu hao waliofunguliwa kwenda kupima tena hospitali na kurejesha majibu kwa ajili ya Ushuhuda.

Tamasha la Usiku wa gospel hiphop lilifanyika siku ya tarehe 27 mei 2016 katika la T.A.G DMC tabata Segerea Chama kuanzia saa tatu usiku hadi asubuhi na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa Rais wa shirikisho la muziki nchini Addo Novemba.

Picha kwa hisani ya Milpa Media

 

Like Page yetu ya facebook >>>> GOSPOMEDIA

Advertisements
Previous post

UFAHAMU UKRISTO NA DINI ZA ULIMWENGU.

Next post

ADDO NOVEMBA KUUNGANA NA YESU OKOA MITAA KUSAMBARATISHA USHOGA