Habari

MWIMBAJI JOSEPH MABULA ANATAFUTA MENEJA WA KAZI ZAKE ZA MUZIKI WA INJILI.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka morogoro Tanzania anayefahamika kwa jina la Joseph Mabula amefunguka leo kupitia tovuti ya gospomedia.com kwamba kwasasa anatafuta msimamizi(meneja) atakayesimamia kazi zake za muziki wa Injili ili aweze kufikisha huduma ya Injili kwa watu wote walio ndani na nje ya Tanzania.

Mwimbaji Joseph Mabula ambaye kwasasa anatamba na wimbo wa Chuki ya Nini ambao unapatikana kwenye tovuti ya gospomedia.com amesema kuwa ili aweze kufanya muziki mzuri wa Injili ni lazima apate utulivvu wa akili kwanza ili aweze kufanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kutunga mashairi yenye ujumbe mzito wa Mungu yatakayogusa maisha ya watu na kuimba kwa kiwango kizuri, hivyo ameona ni heri atafute menejimenti itakayosimamia kazi zake za muziki wa Injili ikiwa ni pamoja na kutangaza na kusambaza kazi hizo ili aweze kufika mbali zaidi ikiwa ni moja ya ndoto alizonazo mwimbaji Joseph Mabula katika Tasnia ya Muziki wa Injili.

Jmabula3

“Kikubwa, niwe na msimanizi wangu wa kunisimamia katika muziki wa injili na kunisambazia kazi ndani ya nchi na nje ya nchi… kusudi niwe na uwezo wa kufikisha huduma kwa watu wote, na niwe na utulivu mzuri wa kutunga nyimbo na kufanya mazoezi..pamoja na kushirikiana na waimbaji wengine nchini hapa nchini na hata nje ya Nchi, Naamini nikiwa na management nzuri naweza kufanya kazi kubwa sana ya Mungu, maana dhamira ni kuhubiri Neno la Mungu kwa watu wa rika zote, hasa vijana maana ndio taifa la leo na sio la kesho nitumike kuwahubiria kupitia uimbaji wangu na kubadilisha maisha yao kutoka kwenye maisha ya dhambi na kuwa wana wapya wanaomtumikia Mungu katika Roho na Kweli” hivi ndivyo alivyosema mwimbaji Joseph Mabula kuhusiana na kuhitaji kupata meneja au msimamizi wa kazi zake. Kwa mdau yeyote anayehitaji kutoa sapoti au kuwa msimamizi wa kazi zake za nyimbo za Injili kutoka kwa mwimbaji Joseph Mabula unakaribishwa na unaweza kuwasiliana naye kupitia:

WhatsApp: +255 656 173 026
Facebook: Joseph Mabula
Instagram:
Email:

Like Page yetu ya facebook >>GOSPOMEDIA.COM instagram> @gospomedia

Advertisements
Previous post

KUTOKUTAJA JINA LA YESU KWENYE NYIMBO ZA INJILI HUO NI UCHANGA WA KIROHO “JOSEPH MALUMBU’

Next post

KAA TAYARI KWA UJIO MPYA WA THE TWINS (MAPACHA) "SIFA ZA BWANA"