Videos

Music Video | Music Audio: Godwill Babette – Egemeo (Moyo Wangu)

Kutoka jijini Nairobi leo kwa utukufu wa Mungu nimekuwekea video ya wimbo wa kuabudu uitwao Egemeo (Moyo Wangu) kutoka kwa mwimbaji mwenye kipawa kikubwa cha uandishi na uimbaji anayefahamika kwa jina la Godwill Babette, video hii imeongozwa na director Bakari Ousman kutoka studio za Crosslife Movement, wimbo ukiwa umeandaliwa na prodyuza Dominic Khaemba.

Hakika utabarikiwa na wimbo huu ambao unazungumzia juu ya kumtegemea Yesu Kristo katika jambo ambalo tunafikiria kufanya kwakuwa yeye ndiye mkuu kupita wakuu wote, yeye ni mfalme kupita wafalme wote, yeye ni Baba.. Kimbilio letu libaki kwake milele.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii nzuri na wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua kwa kadri utakapokuwa unasikiliza wimbo huu na Yesu akawe Egemeo kuu katika maisha yako. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Godwill Babette kupitia:
Simu/WhatsApp: +254 723 159569
Facebook: Godwill Babette Wasidi
Instagram: @godwillbabette
Facebook Page: Godwill babette Ministry

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Music Video | Music Audio: Benachi - Hallelujah

Next post

Music Video | Music Audio: Kambua - Mwaminifu