Music

Music Audio: Vanesa Kasoga – Tangulia

Kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili kutoka jijini Mwanza anayefahamika kwa jina la Vanesa Kassoga leo kupitia tovuti yako pendwa tumekuwekea wimbo wake wa kwanza uitwao Tangulia, ukiwa umefanyika ndani ya studio za Exodus Production chini ya mikono ya prodyuza Kameta kutoka jijini Mwanza.

Tangulia ni wimbo wa sifa unamtukuza Mungu kwa namna ya pekee ukitukumbusha kumtegemea Bwana Yesu ili tuweze kupata nguvu na kibali cha kutenda mambo makuu yanampendeza Mungu.

Hakika hii ni moja ya nyimbo nzuri sana za kusifu ambayo itainua nafsi yako na kukufanya kumfurahia Mungu na kumtegemea Yesu katika kila jambo unalolifanya na hakika utainuliwa na kubarikiwa kwa maana Jina la Yesu litasimama kama nguzo kuu katika maisha yako.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakwenda kubadilisha maisha yako siku ya leo. Mungu akubariki sana unapokwenda kuupokea wimbo huu.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na mwimbaji Vanesa Kassoga kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 756 012 331
Facebook: Vanesa Kassoga
Instagram: @vanesakassoga
Youtube: Vanesa Kassoga

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Music Audio: Lilian Kimola - Umeinuliwa Juu

Next post

Jukumu la Kuliombea Taifa lipo mikononi mwa watanzania wenyewe - Naibu Waziri