Music

Music Audio Music: Paul John – Yesu Asali

Shalom mwana wa Mungu!! leo kutoka jijini Mwanza nimekuwekea wimbo uitwao ”Yesu Asali” kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili akifahamika kwa jina la Paul John, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Apex Music chini ya mikono ya prodyuza Benny William.

Mwimbaji Paul John ni mwimbaji mpya kabisa katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania akiwa chini ya usimamizi wa studio za Apex Music na wimbo huu ni wa kwanza kuachia mwaka huukutoka kwenye studio hiyo.

Yesu Asali ni wimbo unaozungumzia upendo wetu kwa Bwana Yesu Kristo kutokana na yale makuu ambayo ameyafanya na anayoendelea kuyafanya maishani mwetu na sasa ni wajibu wetu kumtukuza na kumsifu kupitia nyimbo na hapa kupitia mtumishi huyu wa Mungu Paul John ametuletea ujumbe wa kutukumbusha nafasi ya Mungu katika maisha yetu na vile tunatakiwa kurudisha shukrani zetu kwakwe ili tuweze kupokea nguvu na baraka ya kuendelea kutenda yale yampendazayo yeye akiwa ni ndio mtawala wetu mkuu duniani na mbinguni.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Paul John kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 759 404 113

Facebook: Paul John
Instagram: @pauljohn
Youtube: Apex Music

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Download Audio Music: Phidelia – Hello

Next post

Tazama Video | Audio Music: Alphee Niyo - Songa Mbele