Music

Music Audio: Lilian Kimola – Umeinuliwa Juu

Kutoka jijini Dar es salaam leo nimekuwekea wimbo wa kukubariki uitwao Umeinuliwa kutoka kwa mwimbaji mkongwe wa nyimbo za Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Lilian Kimola, wimbo huu umefanyika ndani ya studio za  Smart Billionaires chini ya mikono ya prodyuza JB.

Huu ni wimbo wa kusifu na kuabudu unaotukumbusha juu ya kumsifu Mungu na kuhamasisha Imani zetu kuwa na nguvu ya kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo kwa maana yeye ndiye mkuu na mfalme wa anayetawala duniani na mbinguni, sababu ya uhai wetu mpaka leo na vitu vyote uvionavyo duniani ni kwasababu ya upendo wake Yesu kwetu, Tumwinue Yesu naye atatuinua na kutuvusha kwenye mapito magumu ambayo kwa akili zetu za kibinadamu hatuwezi kusimama.

Mungu akubariki sana unapousikiliza wimbo huu na hakika utaweka jambo jipya ndani ya moyo wako na nafsi yako. Karibu ubarikiwe sana.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko wasiliana na mwimbaji Lilian Kimola kupitia:-
Simu/WhatsApp: +255 716 500 009
Facebook: Lilian Kimola
Instagram: @liliankimola
Youtube: Lilian Kimola

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Video Music | Audio Music: PV Idemudia - Asante

Next post

Music Audio: Vanesa Kasoga - Tangulia