Audio

Music Audio: Godfrey Mnakum – Tangulia Mbele

Kutoka jijini Dar es salaam, leo kupitia blog yako pendwa nimekuwekea wimbo uitwao Tangulia Mbele kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili Tanzania anayefahamika kwa jina la Godfrey Mnakum, muziki huu umetayaarishwa na prodyuza Ramso Boy kutoka studio za Life Time.

Tangulia Mbele ni wimbo uliojaa sifa na unyenyekevu wa maombi kwa Mungu maana ulinzi wake katika maisha yetu ndio msingi mkuu wa uhai wetu hivyo kupitia wimbo huu mwimbaji Godfrey Mnakum anatukumbusha kuwa tukimtanguliza Mungu mbele kila kitu kwetu kitakua ni chenye Baraka kwa maana Yesu atakuwa anatawala kila kitu katika maisha yetu, mwana wa Mungu kumbuka kuwa upendo wa Mungu ni mkuu sana kama bado hujaokoka basi muda ni sasa kwa maana Dunia ni mbaya kutembea peke bila Yesu hatari.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha mwana wa Mungu kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao kwa hakika utakwenda kuweka neno la uzima ndani ya moyo wako na hakika Mungu atakuinua.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Godfrey Mnakum kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 758 161 808
Facebook: Godfrey Mnakum
Instagram: @godfreymnakum
Twitter: @godfreymnakum

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Je unazifahamu njia za asili za kukabiliana na kwikwi? Soma hapa ujifunze.

Next post

Audio Music: Shadrack Robert - Nikuimbie