Habari

Milton Mugisha Awa Balozi wa Taasisi ya Karudeca, Wiki Ya Kuweka Akiba Duniani 2017.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Milton Mugisha ambaye kwasasa ni balozi wa Tasisi ya Karudeka leo ametuletea wimbo maalumu uitwao Weka Akiba ikiwa ni wimbo wa kusindikiza wiki ya kuweka Akiba Duniani (World Saving Week) iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali iitwayo Karudeca (Karagwe Rural Development and Environmental Conservation Agency) ikishirikiana na benki ya posta Tanzania TPB.

Akizungumza na gospomedia.com mkurugenzi wa Taasisi ya Karudeca Bw.Steven Revelian alikuwa na haya ya kusema.. ”Baada ya kupata mafanikio mwaka jana, wiki ya Kuweka Akiba Duniani mwaka huu tena inaadhimishwa wilayani Karagwe Tanzania kuanzia tarehe 23 oktoba mpaka tarehe 28 oktoba 2017 katika uwanja wa soka wa Kayanga, Karagwe kuanzia saa 4.00 asubuhi mpaka 10.00 jioni.. na kauli mbiu ya mwaka huu katika Wiki ya Kuweka Akiba duniani (World Saving Week) ni Kuweka Akiba ni Maisha.” Alisema Bw.Stevene.

Bw.Stevene Revelian(kushoto) akiwa mmoja wa wadau wa taasisi ya KARUDECA.

Kwa mwaka huu KARUDECA ndiye mratibu mkuu wa sherehe hii katika maadhimisho ya wiki ya kuweka akiba duniani ikishirikina na wadau wengine ikiwemo Benki ya posta Tanzania (TPB) na Saving Banks Foundation for International Cooperation (SBFIC) ya ujerumani.

Wakati wa maadhimisho ya wiki ya kuweka akiba duniani, KARUDECA na washirika wake wataelimisha jamii ya Tanzania umuhimu wa kuweka akiba kwa siku zijazo na kuwasisitiza wazazi kufungua akaunti za benki kwa watoto wao na wao wenyewe.

Mbali na hayo Taasisi ya Karudeca pia itatembelea shule za msingi na za sekondari kwa ajili ya kutoa elimu hiyo na kufanya mahojiano mbalimbali ya redio ili kupanua wigo wa kutoa elimu ya kuweka akiba kwa watu wote.

Mwimbaji Milton Mugisha akiwa ndio balozi wa taasisi ya Karudeca anakukaribisha kusikiliza wimbo huu ukiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya kuweka akiba duniani(World Saving Week) 2017. Karibu usikilize na upakue wimbo huu ambao ni hakika utapokea jambo la kujifunza siku ya leo.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu taasisi ya Karudeca na Miradi yake kwa jamii wasiliana na mkurugenzi Bw.Steven Revelian kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 752 984 029
Facebook page: Karudeca Tovuti: karudeca.jimdo.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Video | Music Audio: Bertha Kapufi - Maombi

Next post

Neema Ng'asha Kuachia Albamu Mbili Kwenye Tamasha kubwa la Muziki wa Injili, Tar 10 Disemba 2017.