GOSPOMEDIA ni chombo kinachotumika kutangaza Injili kupitia matangazo ya habari kikristo na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Maono

Kuwa chombo bora nchini kinachoitangaza Injili kupitia habari za kikristo na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania, ili Injili hii iweze kubadilisha maisha ya watu wengi duniani kote.

Dhamira

Kutoa huduma bora ya matangazo ya habari za kikristo na burudani za muziki wa Injili, ili kuiwezesha jamii kuipokea Injili na kufunguliwa kiroho.

Chombo cha Gospo Media kimepata kibali cha usajili namba 130837 chini ya kifungu cha sheria ya usajili wa makampuni ya mwaka 2002.

Lengo Kuu

Kufungua kituo bora cha televisheni kitakachokuwa kinarusha matangazo ya habari za kikristo na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania kwa ujumla ifikapo mwaka 2026.

HISTORIA

Gospomedia imeanzishwa mwaka 2013 lilikiwa kama wazo kutoka kwa mwanzilishi wa kampuni hii kijana Ladslaus Milanzi ambaye mwaka 2014 aliamua kutengeneza mtandao wa tovuti ulioitwa gospomuziki.com ukiwa na lengo la kuwasaidia wanamuziki na waimbaji wa nyimbo za Injili kutangaza kazi zao kupitia mtandao huo na ndani ya mwaka huo wa 2014 Ladslaus aliweza kuungana na kijana mwenzake anayefahamika kwa jina la Aloyce Mbezi ambao waliungana na kufanya kazi pamoja na kufikia Novemba 2015 waliweza kubadilisha jina la mtandao wa tovuti hiyo kutoka gospomuziki.com na kuwa gospomedia.com na kufikia novemba 2016 waliamua kusajili kampuni hiyo na kuwa Gospo Media ambayo ilifanikiwa kuisajiliwa rasmi mwaka 2016.

Sababu za kuanzishwa kwa gospomedia

Gospo Media imenzishwa kwa lengo kuu la kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya muziki wa Injili Tanzania ambazo kwa namna moja ama nyingine zimeifanya tasnia hii kutokuwa na muonekano wenye thamani kwa watenda kazi wake wakiwemo wanamuziki na waimbaji wa nyimbo za Injili ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wamekosa jukwaa (platfom) mbadala la kutangaza kazi zao pia changamoto ya wizi wa kazi zao na na hii ni kutokana na aina mifumo iliyopo sasa kutokwenda na wakati na kasi ya teknolojia inayozidi kukua kila siku na hivyo kuzuia fursa mbalimbali kwa waimbaji na wanamuziki katika kutangaza, kusambaza na kuuza kazi zao kitaifa na kimataifa ili kuwaletea maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla hivyo kutokana na changamoto hizi na nyingine nyingi zinazodumaza maendeleo ya muziki wa Injili Tanzania ndizo zilizipelekea kuanzishwa kwa kampuni ya Gospo Media ili kuleta majibu yatakayokuwa suluhisho kwa changamoto hizo na kuifanya tasnia ya muziki wa Injili kuwa na thamani ya juu zaidi katika soko la kitaifa na kimataifa katika sekta ya burudani nchini Tanzania.

Gospo Media ni jukwaa mbadala kwa waimbaji, wanamuziki na watenda kazi wengine wa Injili kuweza kuzitangaza kazi zao kwa upana zaidi kuanzia ngazi ya kitaifa na kimataifa kwa kwenda sambamba na kasi ya Teknolojia ambayo inabadilika na kukua kilasiku.

IDARA NDANI YA GOSPOMEDIA

Kwasasa gospomedia ina mgawanyo wa idara 3 ambazo ni

  1. Idara ya usimamizi (Administration)
  2. Idara ya Habari na Mawasiliano (Information)
  3. Idara ya uzalishaji (Media Production)

UONGOZI WA GOSPOMEDIA

Kampuni ya gospomedia inaongozwa na watu wawili ambao ni Ladslaus Milanzi akiwa ni Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi mtendaji ambaye ni Aloyce Samweli Mbezi ambao wote wapo ndani ya idara ya usimamizi.

Pia gospomedia ina mameneja ambao ni Douglas Kyungai na Joff Mulenga ambao wote wapo ndani ya idara ya uzalishaji(Media Production).

HUDUMA

Licha ya gospomedia kutoka huduma ya kutangaza kazi za waimbaji na wanamuziki wa nyimbo za Injili lakini pia kuna huduma nyinginezo ambazo gospomedia tunazitoa ikiwemo

  • Huduma ya upigaji picha(Photography Service)
  • Utengenezaji wa Matangazo ya graphics

HUDUMA YA MATANGAZO YA MUZIKI WA INJILI

Kwasasa Gospo Media inatoa huduma ya kutangaza nyimbo na video za waimbaji na wanamuziki wa nyimbo za Injili kupitia mtandao wa tovuti ya gospomedia.com ambao umefanikiwa kutembelewa na watu zaidi ya laki 5 toka mwaka 2015 na bado unaendelea kukua zaidi kilasiku.

WASILIANA NASI

Kwa maelezo zaidi kuhusu gospomedia wasiliana nasi kupitia:

Simu: +255658293696

WhatsApp: +255755038159

Facebook: GospoMedia Tz

Facebook Page: GOSPOMEDIA.COM

Instagram: gospomedia

Twitter: GospoMedia

E-mail: [email protected]

Unaweza pia kufika ofisini kwetu Karikoo mtaa wa Tandamti na Kongo Dar es salaam, Tanzania. Karibu sana.