TUZO ZA GOSPO (GOSPO AWARDS) ni tuzo maalum zilizoanzishwa na kampuni ya Gospo Media kwa waimbaji, wanamuziki, na wataarishaji wa kizazi kipya cha muziki wa Injili kutoka Tanzania na Afrika Mashariki walioweza kufanya vizuri kwa mwaka 2016 kupitia tovuti ya gospomedia.com na vyombo vingine vya habari kama vile Radio, Televisheni, mitandao ya kijamii n.k.

Kwa mara ya kwanza tuzo za Gospo zinatarajiwa kutolewa siku ya jumapili ya tarehe 30.04.2017 ndani ya ukumbi wa kanisa la City Christian Center uliopo upanga jijini Dar es salaam kuanzia saa nane mchana na kuendelea.

SABABU ZA KUANZISHWA KWA TUZO ZA GOSPO (GOSPO AWARDS)

 1. Kutambua na kuthamini kazi njema na jitihada za waimbaji, wanamuziki na wadau mbalimbali tasnia ya muziki wa Injili.
 2. Kutoa hamasa na ari kwa wanamuziki na waimbaji wa nyimbo za Injili.
 3. Kuleta mageuzi mapya katika tasnia ya muziki wa Injili Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
 4. Kuongeza chachu ya maendeleo ya ubora wa kazi za wanamuziki na waimbaji wa nyimbo za Injili.
 5. Kupanua wigo wa soko la Muziki wa Injili kutoka ngazi ya kitaifa kwenda kimataifa.
 6. Kutambua na kukuza vipaji vya waimbaji na wanamuziki wapya wa nyimbo za Injili ili kuboresha tasnia ya muziki wa Injili.
 7. Kuhamasisha na kukuza ushirikiano na mshikamano baina ya waimbaji, wanamuziki, na wadau mbalimbali katika tasnia ya muziki wa Injili.

MUDA WA KUTOA TUZO ZA GOSPO

Tuzo za Gospo zitakuwa zinafanyika mara moja kila mwaka chini ya uongozi wa kampuni ya gospomedia ikishirikiana na waimbaji, wanamuziki na wadau mbalimbali kutoka kwenye taasisi, mashirika ya kiserikali na binafsi, makampuni n.k.

UPANA WA TUZO ZA GOSPO

Tuzo za Gospo 2016/2017 itahusisha mikoa yote kutoka ndani ya Tanzania na afrika mashariki kwa ujumla.

 

VIPENGELE VYA TUZO ZA GOSPO (GOSPO AWARDS) MWAKA 2016/2017

 1. Muimbaji bora wa kiume (Best Male Gospel Music Singer of the Year)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji bora wa kiume aliyefanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Muimbaji bora wa Kike (Best Female Gospel Music Singer of the Year)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji bora wa kike aliyefanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Wimbo bora wa mwaka (Best Music Song of the Year)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji aliyefanikiwa kutengeneza wimbo bora na kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Video bora ya mwaka (Best video of the Year)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji aliyefanikiwa kutengeneza video bora na kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Wimbo Bora wa kuabudu (Best Worship Song)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji aliyefanikiwa kutengeneza wimbo bora wenye mtindo wa mahadhi ya kuabudu na kufanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Wimbo Bora wa Gospel HipHop (Best Gospel HipHop Song)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji aliyefanikiwa kutengeneza wimbo bora wenye mtindo wa mahadhi ya gospel-hiphop na kufanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Kundi bora la mwaka (Best Group of the Year)

Ni tuzo itakayokwenda kwa kundi la waimbaji lililofanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Mtaarishaji bora wa Audio (Gospel Music Audio Producer)

Ni tuzo itakayokwenda kwa mtaarishaji bora wa nyimbo za muziki wa Injili aliyefanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Mtaarishaji bora wa Video (Gospel Music Video Director)

Ni tuzo itakayokwenda kwa mtaarishaji bora wa video za muziki wa Injili aliyefanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Album bora ya mwaka (Best Gospel Music Album)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji aliyetengeneza album ya nyimbo na video za muziki wa Injili iliyofanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Muimbaji bora mpya wa mwaka (Best Gospel Music Upcoming Artiste)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji mpya wa nyimbo za Injili aliyejitokeza mwaka 2016 na kufanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Wimbo Bora wa kushirikiana (Best collabo)

Ni tuzo itakayokwenda kwa waimbaji wa nyimbo za Injili walioweza kushirikiana kwa pamoja kupitia wimbo na kufanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Wimbo bora wa mwaka kutoka Afrika mashariki (Best East African Song)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi yoyote zilizo ndani ya afrika mashariki aliyeweza kutengeneza wimbo bora na kufanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Mtangazaji Bora wa Mwaka (Best Gospel Music presenter)

Ni tuzo itakayokwenda kwa mtangazaji wa vipindi vya muziki wa Injili(Radio/Tv) aliyefanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Kipindi bora cha Radio (Best Gospel Music Radio Program)

Ni tuzo itakayokwenda kwa stesheni ya radio inayoendesha kipindi cha muziki wa Injili na kufanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Kipindi bora cha Tv (Best Gospel Music Tv Program)

Ni tuzo itakayokwenda kwa stesheni ya Tv inayoendesha kipindi cha muziki wa Injili na kufanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Management/Label bora ya mwaka (Best Gospel Music Management Label)

Ni tuzo itakayokwenda kwa kampuni au taasisi inayosimamia kazi za wanamuziki wa nyimbo Injili na kufanikiwa kufanya vizuri mwaka 2016 kwa kuzingatia sifa na vigezo vilivyowekwa.

 1. Social Achievement Awards

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji, kikundi cha waimbaji, wachungaji, mhamasishaji(motivational speaker) n.k aliyefanikiwa/waliofanikiwa kubuni vitu na kutekeleza mipango mbalimbali ya kuisaidia Jamii na vitu hivyo au mipango hiyo kuonekana kuisadia jamii kwa kiasi kikubwa hasa vijana.

 1. Tuzo ya heshima (Award of honor)

Ni tuzo itakayokwenda kwa muimbaji/kikundi cha waimbaji wa zamani wa nyimbo za muziki wa Injili na kufanikiwa kufanya vizuri miaka hiyo ya zamani na kuisaidia tasnia ya muziki wa Injili kukua kwa kiasi kikubwa kupitia mchango wa juhudi zao.

 1.  Tuzo Maalum (Special Award)

Ni tuzo maalumu kutoka gospomedia itakayokwenda kwa mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au Taasisi iliyoweza kusaidia na kufanikisha kufanyika kwa tuzo za gospo kwa mwaka 2017 kupitia mchango wa kifedha au huduma.

HATUA ZA KUPATA WASHIRIKI (NOMINEES) NA WASHINDI WA GOSPO AWARDS 2016/2017

HATUA YA KWANZA: Mapitio ya chati za kumi bora.

HATUA YA PILI: Kutangazwa kwa washiriki(Nominees)

HATUA YA TATU:  Kupiga Kura

HATUA YA NNE: Kutangaza washindi wa Gospo Awards 2016/2017

VIGEZO NA MASHARTI YA KUSHIRIKI TUZO ZA GOSPO AWARDS 2016/2017

 1. Wimbo au video ya muimbaji husika ni lazima iwe imefuata misingi ya muziki wa Injili.
 2. Kazi ya Muimbaji ni lazima iwe imekidhi viwango vya ubora kiufundi.
 3. Wimbo au Video ya muimbaji ni iwe walau imetangazwa kupitia tovuti ya gospomedia.com, mitandao ya kijamii, blogs na vyombo vingine vya habari kama vile radio na tv ndani ya mwaka husika.
 4. Wimbo au video ya muimbaji inayotakiwa kushiriki iwe walau imefanikiwa kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali za kumi bora kupitia tovuti ya gospomedia.com, blog zingine za muziki wa Injili, radio na tv.
 5. Washiriki wa tuzo za Gospo Awards ni lazima wawe ni waimbaji, wanamuziki, watangazaji, wataarishaji wa muziki wa Injili na wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla (Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na Congo).

Baada ya sherehe za utoaji wa Tuzo za gospo/Gospo Awards, uongozi na timu nzima ya gospomedia ikishirikiana na wadhamini na wadau mbalimbali itafanya tour maalum ya kuwatambulisha washindi wa tuzo za gospo awards kwenye mikoa mbalimbali Tanzania hii itakwenda pamoja na programu maalumu ya kurudisha shukrani kwa jamii hasa kwa makundi maalumu kama vile watoto waishio kwenye mazingira magumu, wagonjwa walio hospitalini, wazee waliokosa msaada, mama wajane na walemavu lengo la programu hii ni kuikumbusha jamii juu ya kuwajali wengine pale wapatapo baraka za mafanikio.

 

Tuzo za Gospo 2017 zinatarajiwa kutolewa tarehe 30 April 2017 katika ukumbi wa CCC Upanga, Dar es salaam Tanzania.

Kwa maelezo zaidi kuhusu tuzo za Gospo wasiliana nasi kupitia WhatsApp: +255755038159 au piga simu namba +255658293696 au tuandikie barua pepe [email protected] 

Endelea kutembelea tovuti ya www.gospomedia.com kwa habari zaidi.

GOSPO AWARDS 2016/2017 inadhaminiwa na ?