Habari

Goodluck Gozbert Atwaa Tuzo, Sauti Awards 2017.

Muimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Goodluck Gozbert kwa mara nyingine tena ameweka historia katika tasnia ya muziki wa Injili kwa kufanikiwa kutwaa tuzo ya Muimbaji Bora wa kiume Afrika mashariki kwa mwaka 2017 kwenye mashindano ya tuzo za muziki injili nchini marekani zinazojulikana kama Sauti Awards.

katika kipengele hicho mwimbaji Goodluck Gozbert alikuwa akichuana vikali na waimbaji wengine mahiri kama vile Will Paul, Daddy Owen, Exodus, Eko Daydda na Collo.

Hii ni tuzo ya tatu kwa Goodluck Gozbert baada ya kutwaa tuzo mbili kama Msanii Bora wa kiume  na wimbo bora wa mwaka kwenye mashindano ya tuzo za Xtreem Awards mwaka 2015 yaliyofanyika nchini kenya.

Waimbaji wengine ambao wamefanikiwa kutwaa tuzo kwenye mashindano hayo ni pamoja na Mercy Masika ambaye amechukua tuzo ya Muimbaji Bora wa kike afrika mashariki (Best Female East Africa) na Willy Paul akiwa amechukua tuzo ya Video Bora ya Mwaka huku Dj Mo akichukua tuzo ya DJ Bora wa Mwaka kutoka afrika mashariki na waimbaji wengine kadhaa kutoka afrika mashariki.
Sauti Awards ni tuzo zinazotolewa kila mwaka nchini marekani chini ya kampuni ya Sauti One kwa waimbaji wa muziki wa Injili waliofanya vizuri zaidi Afrika

Ikumbukwe kuwa huu ni msimu wa pili kwa tuzo hizi ambazo zimefanyika tarehe 12.08.2017 katika ukumbi wa North Atlanta High mjini Atlanta, marekani.

Uongozi na timu nzima ya gospomedia inapenda kuchukua nafasi hii kutoa pongezi kwa muimbaji Goodluck Gozbert kwa kutuwakilisha vyema watanzania katika tasnia ya muziki wa Injili nchini.

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Music Audio: Kwaya Ya Uinjilisti KKKT Boko - Yawezekana

Next post

Download Music Audio: James Nyambega - Nibariki Hivyo Hivyo