Music

Download Official Music Audio: Juma Kyando – Ni Yesu

Shalom mwana wa Mungu! leo tumekusogezea wimbo uitwao Ni Yesu kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Juma Kyando a.k.a KIBONGE wa YESU, wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Mefo Music Production chini ya mikono ya prodyuza Kingson.

Ni Yesu ni wimbo unaomtukuza Mungu kwa namna ya kipekee kupitia mtumishi wake Juma Kyando(Kibonge wa Yesu) ambaye ametuletea zawadi ya ujumbe wa kiroho uliobebwa kwenye wimbo huu ambao unatukumbusha juu ya ukuu wa matendo ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye aliamua kujitoa na kuteswa ili sisi tukumbolewe na kuwa wapya kwa damu yake iliyomwagika msalabani na kudhihirisha upendo wake wa pekee unaotupatia nguvu ya kumwabudu Mungu na kumtukuza kwa nyimbo za sifa kila siku.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu na ni hakika utabarikiwa. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Juma Kyando(Kibonge wa Yesu) kupitia:
WhatsApp: +255 654 448 206
Facebook: Juma Kyando(Kibonge wa Yesu)
Instagram: @jumakyando_kibongewayesu
Youtube: Juma Kyando(Kibonge wa Yesu)

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Download Audio: Yared Ndolosi - Mshukuruni Bwana

Next post

Kanisa la Askofu Gwajima labomolewa.