Audio

Download Music Audio: Tasha Cobbs Leonard Feat Nick Minaj – I’m Getting Ready

Wimbo uliokuwa unasubiriwa kwa shauku kubwa duniani uitwao “I’m Getting Ready” kutoka kwa mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini marekani Tasha Cobbs Leonard akiwa amemshirikisha Nicki Minaj tayari ameshauachia rasmi ukiwa ni moja ya kati ya nyimbo zilizo kwenye albamu yake mpya iliyoachiwa tarehe 25 Agosti 2017  ikiwa imebeba jina la Heart, Passion, Pursuit. Ushirikiano huu baina ya Tasha Cobbs na Nick Minaj umesababisha vurugu kubwa katika kiwanda cha muziki  wa Injili duniani hasa kwa mashabiki na wadau wa muziki huu Ingawa Tasha Cobbs ameweka wazi upendo wake na shukrani zake za dhati kwa Nicki Minaj na ameahidi kumuweka katika maombi yake ya sala kila siku.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Tasha alisema..

“Nataka kuchukua nafasi hii kumshukuru rafiki yangu @nickiminaj !!! Asante kwa kutangaza sifa zako kwa Mungu ili ulimwengu uweze kusikia na kwa kuweka upendo wako kwa Mungu! Asante kwa kutoa zawadi yako katika albamu hii! Kama nilivyokuwa nakwambia mara nyingi nitasema ili ulimwengu usikie … Nitakuweka milele katika sala! Wengi watabarikiwa na kuwa na Mungu wa kweli kwa sababu uliamua kuchagua kusimama na kufanya rekodi hii..”

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu na hakika utabarikiwa. Karibu!!

Download Audio

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Tazama Video | Download Audio: Elizabeth Kasase Feat Mussa Mazingwa - Usikate Tamaa

Next post

Download Audio: Scola Maghembe Shekidee - Yesu Ametenda Mema