Nyimbo

Download Music Audio: Kwaya Ya Uinjilisti KKKT Boko – Yawezekana

Kutoka jijini Dar es salaam leo tumekusogezea wimbo mpya uitwao Yawezekana kutoka kwaya ya uinjilisti Boko, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Holly trinity chini ya mikono ya prodyuza Regal.

Huu ni wimbo wa kutia moyo sana unaoelezea nguvu za Mungu katika magumu tunayopitia wanadamu kila siku katika maisha yetu hivyo kupitia wimbo huu tunakumbushwa kutokata tamaa katika kila gumu tunalopitia kwakuwa kwa Mungu yote yanawezekana na hakuna linalomshinda hivyo kupitia utunzi wake kwaya hii imesisitiza kuimarisha imani zetu kwa kuwa karibu zaidi na Mungu kupitia sala, ibada na sadaka na Mungu ataweza kuweka nguvu ya uamsho na kushinda kila jaribu.

Kwa unyenyekevu mkubwa tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu mzuri ambao tunahakika utakubariki na utakwenda kuimarisha imani yako na katu usikate Tamaa. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na kwaya hii ya uinjilisti Boko kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 715 710 186 au +255 784 252 525
Facebook: Kwaya ya Uinjilisti Boko KKKT
Instagram: @uinjilistikwaya.bokokkkt

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Audio: Paul Nhiga - Pendo Lako

Next post

Goodluck Gozbert Atwaa Tuzo, Sauti Awards 2017.