Music

Download Music Audio: Christopher Mwahangila – Mungu Hawezi Kukusahau

Bwana Yesu asifiwe mwana wa Mungu! leo kupitia blog yako pendwa tumekusogezea wimbo uitwao ”Mungu Hawezi Kukusau” kutoka kwa mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini Tanzania anayefahamika kwa jina la Christopher Mwahangila ambaye kwasasa amekuja na album yake mpya inayobeba jina hilo la ”Mungu Hawezi Kukusahau” ikiwa ni albamu yake ya nne yenye mkusanyiko wa nyimbo saba na ikiwa inapatikana kwenye mfumo wa Audio CD kwenye maduka yote ya wasambazaji wa albamu za muziki wa Injili nchi nzima.

Mungu Hawezi Kukusau ni wimbo wa baraka sana unaotia moyo na kutoa nuru ya matumaini kwa watu wanaopitia changamoto mbalimbali za kimwili na kiroho na leo kupitia mtumishi wa Mungu Christopher Mwahangila ametuletea ujumbe wa faraja juu ya kumtegemea Mungu kwa maana yeye Hawezi Kutusahau katika kila jaribu unalopitia Mungu atakupigania.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utabarikiwa na kuinuliwa.

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi au mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Christopher Mwahangila kupitia
Simu/WhatsApp: +255 716 620 000 +255 756 068 844
Facebook: Christopher Mwahangila
Instagram: @christophermwahangila

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Tazama Video | Download Audio: Jerry K - The Air I Breath

Next post

Tazama Video | Download Audio Music: Mutale Nkonde - Make a Difference