Audio

Download Audio: Shadrack Ngailah – Macho Ya Roho

Kutoka jijini Arusha, leo tunamleta kwako muimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Shadrack Ngailah na leo kupitia blog yako pendwa ya gospomedia tumekusogezea wimbo wake mpya uitwao Macho ya Roho ukiwa ni wimbo unaobeba jina la album yake ya kwanza iitwayo ”Macho ya Roho” .

Katika wimbo huu muimbaji Shadrack ametukumbusha juu ufunuo wa macho ya rohoni unavyoweza kumsaidia binadamu hasa yule anayeamini kufunuliwa kiroho na kuona vitu ambavyo vipo kwenye ulimwengu wa kiroho, hivyo kupitia wimbo huu Shadrack amesisitiza kufanya maombi na ibada mara kwa mara ili tuwe karibu na uwepo wa Mungu ili kupitia roho mtakatifu tuweze kufunuliwa na kwenda kinyume na mabaya yote ambayo yanaweza kuwa kikwazo cha kuufikia utukufu wa Mungu Baba.

Kwa moyo mkunjufu gospomedia.com tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao hakika utafanya siku yako iwe ya baraka sana baada ya kusikiliza. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi ya jinsi ya kuipata album yake na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Shadrack Ngailah kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 768 778 682
Facebook: Shadrack Ngailah
Instagram: @shadrackngailah

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Music Audio: Gelax Wakristo Feat. Henry Ngosi - King'ora

Next post

Tazama Video | Download Audio: Milca Kakete - Siku Imeanza