Music

Download Audio: Paul Nhiga – Pendo Lako

Kutoka jijini Dar es salaam leo tumekusogezea wimbo mpya uitwao Pendo Lako kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Paul Nhiga. wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Relight.

Huu ni wimbo wa Ibada ukiwa umeandikwa na Paul Nhiga ukieleza ni namna gani pendo la Mungu ni kuu, linadhihirika hata kwenye mapungufu yetu, mtunzi Paul Nhiga amejidhihirisha mwenyewe kupitia utunzi wake namna anavyofurahia kupendwa na Mungu pamoja na mapungufu yake aliyonayo lakini Mungu akimtizama anamwona kakamilika tofauti na binadamu watizamavyo.  Hakika huu ni wimbo ambao pia umelenga kumuunganisha kila mtu kwa Mungu na kumtafakari kwa namna atakavyoguswa.

Kwa moyo wa unyenyekevu blog yako pendwa ya gospomedia inakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu mzuri kabisa ambao tunahakika utakubariki na kukuinua sana. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Paul Nhiga kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 764 783 793
Facebook: Paul Nhiga
Instagram: @paulnhiga
Youtube: Paul Nhiga

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram: @gospomedia

Lads

Lads

Naitwa Ladslaus Milanzi, mwanzilishi na msimamizi wa tovuti hii ya habari za kikristo, nyimbo na video za muziki wa Injili, Asante kwa kutembelea tovuti hii nikiamini kuwa umebarikiwa na kufurahia na vyote ambavyo umevipata kupitia tovuti hii ikiwa ni moja ya chombo kilichobeba kusudi la kuieneza Injili na kuihudumia jamii kupitia habari na burudani. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Download Audio: Rungu la Yesu - Uandishi na Flow

Next post

Download Music Audio: Kwaya Ya Uinjilisti KKKT Boko - Yawezekana