Music

Download Audio Music: Matto Cole – Grown

Kutoka mjini London Uingereza mpaka Tanzania leo tumekuwekea wimbo uitwao Grown kutoka kwa mwimbaji Matto Cole ambaye ni mzaliwa wa nchi ya Sierra Leone.
Huu ni wimbo unaozungumzia jinsi maisha yetu yanavyopitia hali ya magumu kila wakati, na wakati mwingine unahisi kama huwezi kufanikiwa lakini kupitia wimbo huu mwimbaji Matto Cole anatatukumbusha kuwa Ikiwa unamwamini Yesu Kristo inawezekana kushinda changamoto na vikwazo vyote vinavyokusuma chini, na unapofika wakati unaofaa kwako, utaelewa kwa nini ulipaswa kupitia magumu hayo katika maisha yako.
Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu amabo ni hakika utakubariki na kukuinua siku ya leo. Karibu!!

Social Media
Facebook: Matto C
Instagram: @mattocole
Twitter: @mattocole

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Lads

Lads

Mimi ni Ladslaus Milanzi mwanzilishi na muasisi wa mtandao bora wa habari za kikristo, maarifa na burudani za muziki wa Injili kutoka ndani na nje ya Tanzania. Naamini nimebeba kusudi la kumtumikia Mungu na jamii kupitia chombo hiki ambacho kwa hakika kinazidi kuwa baraka kwa waimbaji, wachungaji, watu binafsi, makanisa na taasisi mbalimbali ambazo zimekuwa zikitumia chombo hiki kupata taarifa, kujifunza na kujitangaza. Mungu Ibariki Gospo Media, Mungu Ibariki Tanzania.
Wasiliana nami kupitia simu/whatsApp: +255 755 038 159.

Previous post

Bahati Simwiche Kuweka Wakfu Albamu Yake Mpya Tarehe 8 Oct. 2017 C.A.G Gongo la Mboto.

Next post

Tazama Video | Download Audio: Beda Andrew - Nitakuwa na wewe