Audio

Download Audio Music: Enea Mahenge – Nina Deni

Kutoka jijini Dar es salaam leo tumekusogezea wimbo uitwao Nina Deni kutoka kwa mtumishi wa Mungu Enea Mahenge, wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za BackYard chini ya mikono ya prodyuza Kidaso.

Nina Deni ni wimbo unaokiri Imani ya kweli kwa kumtukuza Yesu Kristo kwakuwa amekuwa mwokozi na mwanga wa maisha yetu kupitia mambo mema anayoendelea kututendea kila siku na kupitia wimbo huu mwimbaji Enea Mahenge anathibitisha kupokea ushuhuda wa kupata ukombozi kutoka kwenye majaribu aliyokuwa nayo mara baada ya kumkabithi Yesu maisha yake na sasa amesikia ndani ya roho yake kuwa kuna deni la kumshukuru na kumtumikia Mungu kwa kutangaza neno na sifa zake na hii ndio maana halisi ya kuachia wimbo huu ambao hata wewe utakayesikiliza utabarikiwa.

”Kunapokua na ushuhuda fulani ambao Mungu amekutendea na kuuona wazi ushuhuda huo ndipo unapojikuta una deni linalokuhitaji kumtumikia Mungu kwa kumshukuru na kutangaza neno lake mahali pote duniani kwakuwa naamini kuna watu wengi bado hawajazijua habari za Yesu Kristo na nafasi yake katika maisha yao”, Alisema mwimbaji Enea Mahenge.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakwenda kuwa baraka kwako na kwa wengine wote. Karibu!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Enea Mahenge kupitia:
WhatsApp: +255 759 554 943
Facebook: Enea Mahenge
Instagram: @eneamahenge
Youtube: Enea Mahenge

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Audio Music: Anicia Kinemo - Ushuhuda Wangu

Next post

Download Audio: Fidelis Njocomeon - Kindumbwe Ndumbwe