Audio

Download Audio Music: Benny William – Nakupenda

Shalom mwana wa Mungu!! leo kutokea jijini Mwanza nimekuwekea wimbo uitwao Nakupenda kutoka kwa mwimbaji mpya wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Benny William, wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio za Apex Music chini ya mikono yake mwenyewe akiwa ndiye prodyuza wa studio hiyo.

Nakupenda ni wimbo unaomsifu Mungu katika viwango vya juu, ambapo kupitia mtumishi wake Benny William anatukumbusha Upendo wetu kwa Yesu Kristo ambaye ametupenda hata kabla ya kuumbwa kwetu na hata baada ya kujitoa ili ateswe na kufa msalabani bado anaendelea kutupenda hivyo ni nafasi yetu sasa kila mmoja kujitathmini na kurudisha upendo kwa Mungu kupitia ibada na matendo matakatifu yampendazayo yeye maana hata pumzi na uhai wetu ni kwasababu ya upendo wake, hakika huu ni wimbo wa kubariki sana ambao utakuinua na kukupeleka mahali palipo na uwepo wa Mungu.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao utakwenda kuachilia baraka kwako siku ya leo na siku zote utakapoendelea kuusikiliza. Karibu ubarikiwe!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na muimbaji Benny William kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 719 813 124
Facebook: Benny William
Instagram: @bennywilliam_Official
Youtube: Ben William

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Mwimbaji Ritha Komba Kuja na Video Mpya Mwezi Oktoba, ''Nitashinda''.

Next post

Tazama Video | Download Audio Music: Tukuswiga IM - Usiniache