Audio

Download Audio: Chris Shalom – Your Word Is Truth

Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili nchini nigeria Chris Shalom ameachia wimbo wake mpya uitwao ”Your Word Is Truth” (Neno lako ni kweli) ukiwa ni mfululizo wa nyimbo anazoendelea kuziachia mwaka huu na hii ni baada ya kuachia wimbo wake uitwao “Dry Bones are Rising” kutoka kwenye album yenye mfululizo wa nyimbo hizo iitwayo “Worship in Every Place”

Katika wimbo huu wa ”Your Word Is Truth” (Neno lako ni kweli) Chris Shalom anazungumzia uhakikisho wa neno la kinabii. Katika ulimwengu unaoonekana kama umechanganyikiwa, mtu anaweza kuamini uongo kwa sababu ya hali na majaribu, lakini kama utasimama katika sheria kamili ya Mungu, utapata tumaini na kupata nguvu ya kushinda changamoto za kutisha. Neno la Mungu ni jibu kwa swali lolote.

“Neno ni kweli, Neno ni mamlaka ya mwisho, Neno ni nguvu ya Mungu, Neno ni hai na hai.” Neno ni akili ya Mungu. “Neno ni utoaji wa Mungu kwa wanadamu. Neno ni amani Neno ni upendo.Neno ni uzima. Neno ni uongozi “- Chris Shalom. baadhi ya mistari inayopatikana kwenye wimbo huu.

Kwa moyo mkunjufu tunakukaibisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utabariki na kukuinua. Karibu!!

Download Audio

Social Media:
Facebook: Chris Shalom
Instagram: @chrisshalom_thegoldenvoice
Twitter: @shalom_chris
Web: chrisshalomonline.com

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Uchaguzi Mkuu CHAMUITA kufanyika Tarehe 29 Septemba 2017.

Next post

Tazama Video | Download Audio: Judia Amisi - Ni Neema