Audio

Download Audio: Agent Snypa – Unconditional

AgentSnypa, malkia wa muziki Injili katika miondoko ya Reggae Dancehall kutoka nchini nigeria anakukaribisha kusikiliza wimbo wake mpya uitwao UNCONDITIONAL ukiwa umetayarishwa na prodyuza Ace.

AgentSnypa aliachia album yake ya kwanza mwaka 2015 ambayo ilibebwa na wimbo uliofanya vizuri kwa kiasi kikubwa uliofahamika kwa jina la “High Grade” na baada ya kukaa kwa muda mrefu sasa amekuja na wimbo wake mpya wenye mahadhi Reggae Dancehall, ukiwa umebeba ujumbe wa kiroho, aina ya muziki aliotumia katika wimbo huu utakufanya usiache kuendelea kusikiliza wakati wowote.

Wimbo huu umeguswa na baadhi ya maandiko kama vile Yohana 3:16, Mithali 10:22 na amezungumzia juu ya kumshukuru Mungu kwa yale aliyomtendea kwa upendo na baraka zake bila masharti juu yake.

gospomedia.com inakukaribisha kushiriki upendo wa Mungu kwa kusikiliza na kupakua wimbo huu. Barikiwa!!

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na Agent Snypa

Facebook: Grace Faridah
Kingschat: agent snypa
Instagram: @agentsnypa
Twitter: @agentsnypa

Like Page yetu ya facebook >> GOSPOMEDIA.COM instagram>> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Download Audio: Shonaman - High Five

Next post

Madam Flora Atema Cheche Kwa Wanaomchafulia Jina lake Mitandaoni