Audio

Audio Music: Pompi – Kapena

Akiwa bado anaendelea kufurahia mafanikio ya wimbo wake wa kwanza uitwao “Silence” aliouachia wiki chache zilizopita mwimbaji Pompi kutoka nchini zambia ameachia tena wimbo wake mwingine uitwao ”Kapena”.

“Kapena” ni neno lenye asili ya lugha ya Nyanja huko nchini zambia ikiwa na maana ya ”AU”, Huu ni wimbo unaomhusu mtu ambaye ameamua kuchukua hatua zaidi katika misingi aliyoijenga katika moyo wake na anaamua kuingia katika mahusiano na kumwamini msichana anayempenda. lakini kumbukumbu zake bado zinarudi nyuma kwenye mahusiano ambayo yalimpa mateso na kusumbuka sana lakini sasa amekutana na msichana ambaye amemfanya kuwa tayari kuingia naye kwenye ndoa, Kupitia wimbo huu mwimbaji Pompi anawaasa vijana hasa wale ambao wameumizwa kwenye mahusiano kwamba bado wana nafasi ya kuanza upya kikubwa wazidi kuwa karibu na Mungu ili wapate kibali cha kuwa na macho ya rohoni na kuwatambua wale wanaofaa kuwa nao katika safari yao ya maisha.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utabarikiwa. Karibu!

 

Download Audio

Social Media:

Facebook: The Pompi
Instagram: @thepompi
Twitter: @thepompi

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Music Video | Music Audio: Same OG – Power

Next post

Music Audio: Richard Petro - Hashindwi