Audio

Audio Music: Kenny Rich – Njaa Kali

Baada ya kuachia wimbo uitwao Mkanye leo kwa mara nyingine tena nimekuwekea wimbo uitwao Njaa Kali ukiwa ni wimbo mpya kabisa kutoka kwa mwimbaji anayekuja kwa kasi katika kiwanda cha muziki wa Injili Tanzania akitokea jijini Arusha, na mwimbaji huyu si mwingine  bali ni Kenny Rich au unaweza kumwita Kennedy Richard, wimbo huu umetayaarishwa ndani ya studio za Treestar zilizopo jijini Arusha.

”Katika maisha yetu ya leo kuna wakati mwingi tunakuwa na njaa ya neno la Mungu, japo tunaweza kuwa na kila kitu katika maisha ila bila neno la Mungu bado mambo hayawezi kuwa sawa na kamilifu na hapo ndipo tunahitaji neno la Mungu ili tupate afya ya uzima wa kiroho.” – Kenny Rich.

Kenny Rich ni moja ya waimbaji walio chini ya menejimenti ya Treestar Promotions yenye jukumu kubwa la kutambua na kuviendeleza vipawa vya waimbaji wapya wa muziki wa Injili mkoani Arusha ikiwa tayari na mpaka sasa imekuwa inawasiaidia waimbaji kadhaa ambao tayari kazi zao zimeanza kuonekana na kuwabariki watu wengi.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki sana siku ya leo.

 

Download Audio

Kwa mawasiliano zaidi na huduma ya mialiko wasiliana na mwimbaji Ken Rich kupitia:
Simu namba/WhatsApp: +255 656 450 681
Instagram: @kennyrich_tz
Youtube: Tree Star Promotions

Like facebook page >> GOSPOMEDIA  Follow instagram page >> @gospomedia

Advertisements
Previous post

Audio Music: Voke – We Are Human

Next post

Audio Music: Emem Washington Feat. Morayo – Rebirth